Angel - Sehemu ya Kumi na Sita (16)
Wakafika mpaka sokoni.
Huko walinunua mahitaji waliyotakiwa kununua kama kawaida yao na kufungasha.
Sasa kimbembe kikazuka kwenye swala la kurudi nyumbani.
Agnes alianza tena mada kama za siku iliyopita.
Alisema yeye alikuwa anahitaji kupitia tena kule hivyo Angel amsindikize.
“Tena?”
Angel aling'aka.
“Kwahiyo hautaki au?”
Agnes akauliza.
“Ndiyo mimi siwezi kwenda huko wewe nenda tu mi narudi nyumbani.”
Angel akasema hivyo.
“Nenda...”
Agy akajibu kifupi kuashiria alikasirishwa na maamuzi ya Angel.
Angel hakukopesha waliachana pale pale yeye akashika njia ya kurudi nyumbani wakati huo Agnes yeye akienda anakokujua yeye.
Kwa kuwa mazingira alishayakariri basi ikawa rahisi kwake kufika mapema nyumbani.
Cha ajabu alikuta mlango uko wazi.
“Mh! Inamaana Agy keshafika sasa hivi?”
Alijiuliza Angel.
Akilini alijua itakuwa Agnes ndiye aliefungua huo mlango kwani kama ni shangazi yake Rebecca alikuwa ameshakwenda
kazini na isingekuwa rahisi tena muda huo awe nyumbani hapo.
Akafika mpaka mlangoni, mara akasikia sauti ikitokea ndani ikisema...
“Ndiyo kwa milioni 30 hapo sawa.”
Ilikuwa ni sauti ya Rebecca na ilionekana alikuwa akiongea na simu na simu yenyewe ilikuwa ni ya ishu nzito.
Pale Angel akapata wazo la kunyata mpaka karibu na chumba cha shangazi yake ili aweze kusikia alikuwa akiteta kuhusu nini?
Akafanikiwa kufika mpaka karibu kabisa na chumba hicho pasipo kustukiwa akaweka kambi hapo huku akitega masikio yake vyema kama antena.
“Yaani ushindwe wewe tu, huyu bado mbichi kabisa jana nilimtuma mfanyakazi wangu wa ndani akamchunguze
viungo vyake wakati wa kuoga, aliniletea majibu kuwa yaani uwanja wake ulikuwa ni mpya kabisa.”
Alisema Rebecca huko chumbani...
“Mmh!”
Angel nae akaguna kimyomoyo huku, ni kama alishitukia kitu vile.
“Basi sawa, baadae tuwasiliane.”
Rebecca akahitimisha kuongea na simu kihivyo, halafu kwa bahati mbaya Angel hakubahatika kumsikia mtu wa upande wa pili.
Simu ikakata lakini dakika moja ikaita tena.
“Mmh inaita tena?”
Alijisemea Angel huku akiongeza umakini kusikia nani anampigia Rebecca tena.
Akapokea...
“Hallo Agy.”
Angel akashituka baada ya kugundua mpigaji ni Agnes, akazidi kutega masikio yake kusikia wanataka kuongea nini?
“Tena?”
Rebecca alionekana kutaharuki kuashiria kuna taarifa mbaya alipewa.
“Hapa sizani kama keshafika maanake mi nipo chumbani huku.”
Kusikia hivyo Angel akajua anaezungumziwa ni yeye, mapigo ya moyo yakaanza kumwendea mchaka mchaka.
“Sawa ngoja nitoke nimwangalie huko nje.”
Akajibu Rebecca.
Angel hakutaka kukutwa pale sebleni, akatelezea nje fasta.
“Sasa huyu ngoja nimuuze nitajifanya kama ndiyo narudi sasa hivi.”
Alijisemea kimyomoyo Angel kisha akapitia uchochoro flani hivi na kwenda kutokea njiani mbali kidogo na nyumbani kwa Rebecca.
Akaanza kuja tena!
Unaona akili hiyo?
Akafika tena mpaka nyumbani hapo na kumkuta Rebecca akiwa nje na simu yake mkononi.
Kwa mwendo wa taratiibu Angel akakaribia mpaka mahali alipokuwa amesimama shangazi yake Rebecca.
“Sasa mwenzako yupo wapi?”
Lilikuwa ndiyo swali la kwanza kutoka kwa mwanamke huyo.
“Nimemwacha huko.”
Angel alijibu huku akiangalia chini.
“Kwanini mmeachana tena? Kwani si mlitoka pamoja??”
Akauliza.
“Ndiyo tulitoka pamoja.”
Angel akajibu.
“Sasa kilichowaachanisha ni kipi?”
“Nimeona Agnes ameanza mizunguko yake ambayo mimi hainihusu.”
Akajibu Angel huku akianza kuondoka taratibu.
Rebecca akakosa cha kuzungumza hivyo Angel akaondoka zake.
Lakini pia upande wa pili alifurahi kwa kujipa matumaini kuwa Angel hakusikia mazungumzo yake kwani aliamini
kweli Angel alikuwa ndiyo anafika, asijue kuwa kuna usanii umefanyika!
Mchana wa siku hiyo...
“Sikia nikwambie Angel.”
Ilionekana kuna jambo Rebecca alitaka kumwambia Angel.
Ilikuwa ni katika bustani moja nzuuri sana iliyopo nyuma ya nyumba yake.
Angel na Rebecca walikuwa wameketi kule baada ya chakula cha mchana.
“Nakusikiliza Shangazi.”
Angel akajibu kwa sauti ya upole iliyojaa unyenyekevu.
“Ninakupeleka shule lakini naomba nikwambie kitu kimoja.”
Akasema.
“Kitu gani hicho Anti?”
Akauliza Angel.
“Hivi ni kweli wewe ni bikra?”
Akauliza tena!
“Anauliza bikra yangu ya nini huyu?”
Akajiuliza Angel kabla ya kujibu.
“Ndiyo Anti Rebecca.”
“Kweli?”
“Ndiyo kwani vipi?”
“Sikiliza nikwambie.”
Akasema hivyo huku akimsogelea karibu zaidi.
“Kwenda shule na bikra ni hatari sana walimu au wanafunzi wa kiume wakikugundua watakubaka tena watakuumiza siyo
kidogo nakushauri itoe kabla hujaanza masomo.”
Rebecca aliongea maneno ambayo kwa Angel aliyaona ni ya ajabu sana.
“Hapana! Anti sitobakwa na wala sitoipoteza kwa wakati huu.”
Angel akajibu.
“Utabakwa Angel nisikilize mimi.”
Alisisitiza sana Rebecca.
“Sitobakwa niamini mimi Anti sipo tayari kabisa kuupoteza uschana wangu bila malengo.”
Angel alijibu kwa kujiamini mno, jambo lililoanza kumpandisha hasira Rebecca aliona sasa wanakoelekea atakosa mkwanja.
Maanake hapo ana dili lake ambapo Angel akikubali tu anavuna mpunga mrefu sana.
“Unajua nini Angel, kuna tajiri mmoja anatafuta bikra sana yupo tayari kutoa shilingi milioni thelathini kwa
yeyote mwenye nayo sasa kwanini usichangamkie fursa hiyo?”
Alisema Rebecca.
Pale pale akakumbuka…
“Ndiyo kwa milioni 30 hapo sawa.”
Aliyakumbuka maneno yale...
“Kuumbee! Ndiyo huyu ee? Sasa sikubali.”
Unaweza pia kusoma: