Angel - Sehemu ya Ishirini na Sita (26)
Haraka sana yule mwanaume akaondoka na kwenda kupanda gari yake tayari kwa kumfuatilia Angel.
“Daah! Huyu ni mmoja kati ya wadau wangu wa damu kabisa ngoja nimpe hii kabla ya kuendelea na safari yangu.”
Kijana mmoja aliekuwa safarini kutoka Dar kwenda Iringa alijisemea baada ya kumuona Angel akiwa barabarani.
Kwa kuwa alimwonea mbali kidogo basi taratibu alianza kupunguza mwendo wa gari yake ndogo na ya kifahari aina ya
“Toyota Land Cruiser.”
Akafika mpaka karibu kabisa, akafunga breck na kusimama.
Nusura Angel akurupuke baada ya kugundua gari ile ilisimama kwa kusudi yake lakini akaona tayari amekwisha chelewa kwani hata
kama ataanza kukimbia haitosaidia kitu atakamatwa tu!
Kijana kashuka…
Aaah!
Mtu mwenyewe siyo mgeni kabisa machoni, anakumbuka ni kama aliwahi kumuona mahala ila hamkumbuki kabisa kama ni nani?
“Hey! Vipi?”
Alisalimia huku akirusha mikono yake huku na kule.
“Safi.”
Angel akajibu kifupi huku akiwa makini na mtu huyo.
“Inaonekana wewe ni shabiki wa Andrea Stephano Jr. siyo? Or Simulizi za Andrea.”
“Kwanini unauliza hivyo?”
“Hii T_shirt uliyoivaa si ina chapa yake hapa kifuani?”
Wakati huyo jamaa anazungumza hayo alikuwa hajamtizama Angel vizuri usoni.
“Ni kweli... Hii T_shirt niliinunua tu ingawa huyo mtu hata simjui vizuri kwani hata simu ya kuingia
mtandaoni sina, kwani nasikia ni moja kati ya mastaa wa simulizi mtandaoni.”
Angel alizungumza kwa uchangamfu mkubwa sana, hakutaka kuonesha matatizo aliyonayo.
“Sasa ulisikia au kuona wapi? Kama mtandaoni haupo?”
Alizungumza hivyo wakati huo akiyumbishia mboni zake kwenye uso wa mschana huyo!
Ooh!
Akashituka, ni kama alikumbuka kitu hivi...
Lakini akatulia kwanza.
“Niliwahi kusikia simulizi yake moja ikisimuliwa redioni, ilikuwa ni simulizi nzuri mno niliifwatilia kwa karibu sana.
Kila siku bila kukosa mpaka inafika tamati, siku ya mwisho ndiyo mtangazaji akatoa tangazo la Tishet hizi na sifa zake...
Sikuwa na pesa ya kununulia tisheti hizo, ikabidi nimlilie mama mpaka akafuatilia na kuninunulia...
Hakika nilifurahi sana.”
“Hebu.... Unaitwa Angel.”
Dooh!
Butwaa alilopigwa nalo Angel halikuwa na mfano, hofu na hisia mbaya juu ya mtu huyo vikaanza kujenga kibanda moyoni.
“Mimi ni Jr. hebu nitizame vizuri unikumbuke!”
Pale pale Angel akakumbuka baada ya kumtizama kwa makini kijana huyo, alikumbuka mara ya mwisho waliachana ubungo.
“Uliniambia unakwenda kwa shangazi yako kusalimia siyo?”
“Ndiyo ni mimi Jr.”
Alijibu Angel huku taratiibu lile tabasamu alilokuwa nalo dakika kadhaa lilianza kuyeyuka taratibu usoni kwake
mithili ya bonge la barafu liwekwapo juani.
“Ahaa! Ok sawa, sasa mimi ndiyo huyo mtunzi, nimejitambulisha kwako kifupi kama Jr.
Hata siku hiyo nilijitambulisha hiyo hivyo.
Niliona umevaa Tisheti hii nikatambua kuwa wewe ni mmoja kati ya wale mashabiki wangu wa damu, nikaamua nisimame nikupe
walau salamu, lakini pia nashukuru kukutana na wewe kwa mara ya pili.”
Jr. Aliongea hivyo huku akionesha dalili za kutaka kuondoka.
“Samahani kaka angu.”
“Ooh! Bila samahani dada Jr. Nipo hapa.”
“Ninahitaji kufika Morogoro leo leo kuna matatizo yananiandama naomba unisaidie hata elfu kumi tu ya kuombea lifti maana kwa nauli haitoshi.”
“Matatizo? Yapi tena hayo?”
“Muda hautoshi kukueleza, nitaomba unipatie namba yako siku nikitulia nitaazima simu, nitakupigia kaka angu nikueleze.”
Jr. Akatulia kwa muda huku akimsoma Angel usoni kubaini kama kile anachokizungumza kina uhalisia?
Macho ya Angel yalidhihirisha kuwa ni kweli alikuwa na matatizo makubwa sana.
“Ok... Pole sana, ingia kwenye gari yangu nikufikishe huko uendako kwa maana mi nakwenda Iringa.”
“Samahani.... Gari yako sitoweza kupanda kwani wenda nikakuambukiza matatizo kaka angu samahani kwa hilo?”
“Matatizo? Kwani unatafutwa?”
“Ndiyo ninatafutwa sana tena saana na polisi.”
“Ee!”
Alitahamaki...
“Kwa kosa gani kubwa ulilolitenda binti mdogo kama wewe?”
“Sijatenda kosa lolote zaidi ya kuonelewa tu.”
“Sasa unatafutwa kwa kosa gani la kuonelewa?”
“Ni stori ndefu sana, ila kiufupi ni kwamba shangazi ananilazimisha nikae kwake ili anifanyie ukatili wa
kijinsia.
Hili limenikosa mpaka mara mbili.
Nimeamua kutoroka sasa ameamua kutumia nguvu ya dola kunisaka na sijui amewaambia nini polisi na sijui nikikamatwa nitaishi mazingira gani.”
Angel aliongea huku machozi yakimtoka kabisa...
“Kwani we hauna wazazi wako ambalo labda wangekuwa wanaifahamu tabia ya mwanamke huyo kabla ya wewe kwenda?”
Kabla Angel hajajibu swali hilo, kuna gari ndogo aina ya VX Ilikuja kwa kasi ya ajabu na kupita...
Lakini hatua kadhaa ilisimama...
Anashuka mwanaume ambae baada ya kushuka tu Angel alimtambua mara moja!
Alikuwa ni yule mwanaume aliekuwa akiwasiliana na Rebeca kule ubungo.
“Nimekamatika.”
Angel alijisemea hivyo huku moyo ukianza kumwendea mpute mpute!
Hakuweza kufanya chochote mpaka mwamaume huyo anawafikia pale...
“We binti upo chini ya ulinzi, hauruhusiwi kunyanyua hata kidole!”
Mwanaume huyo alitema mkwara mkali huku akitoa bastora yake mfukoni na kumnyoshea Angel kichwani...
Jr. Mwenyewe alibaki meno nje asijue nini afanye, aondoke au?
Taratibu mwanaume huyo anatoa simu yake na kumpigia Rebeca…
“Nimekwisha mweka chini ya ulinzi wahini.”
Mwanaume huyo alizungumza kifupi tu kisha akatoa simu sikioni.
Wakati jamaa huyu anaongea na simu hiyo vilisikika ving'ora vya magari ya polisi kupitia simu yake...
Hii iliashhria kuwa yule aliekuwa akiongea nae alikuwa ndani ya msafara wa polisi.
“Oo my god... Angel mimi nimekwisha lo!”
Angel alianza kujinung'unikia huku akijuta kupoteza muda kumusikiliza kijana yule pangine hata asingekuwa hapo.
Hapo sasa ndipo Jr alipogundua kuwa ile ishu haikuwa ya kitoto pale ndipo alipoipata na ile akili ya uthubutu akajaribu kuongea na mwanaume yule.
“Samahani braza kwani huyu binti ana kosa gani?”
Aliuliza Jr huku akikutanisha viganja vyake.
“Aah! Hilo mimi halinihusu hapa mi ninachojali ni kazi nimepewa kazi ya kumkamata huyu hivyo kushughulika na kosa lake siyo kazi yangu.”
Mwanaume huyo alitoa jibu la kukatisha tamaa kabisa…
“Sikia kaka huyu binti hajafanya chochote i…”
“Stooop! Unataka kuongea nini hapa?”
Akaja juu kama moto wa mabua...
“Ninachotaka kuongea kinaweza kuwa na point zaidi ya kile ukifanyacho wewe!”
Akajibu Jr kwa kujiamini…
“Aisee! Dogo fanya uchome kiatu kabla mambo hayajakugeukia sawa?
Huyu kama ni demu wako utamfuata kituoni tunaelewana?
Staki ujinga.”
Angel alikuwa akiyasikia maneno yale hakika aliumia mno.
Aliamini kuwa Rebeca alimlipa pesa nyingi sana mwanaume huyo kwahiyo isingekuwa rahisi kumsikiliza mtu yeyote yule.
Sasa nini kifanyike kabla mambo hayajaharibika?
Jr taratibu akageuka na kuanza kuelekea kwenye gari yake...
Unaweza pia kusoma: