Muonekano wa Giza:

Msaada

Angel - Sehemu ya Nane (08)

Hata hivyo alishindwa kumpatia jibu sahihi kwani pindi alipojaribu kufanya hivyo alikutana na tabasam paana usoni kwa babu yake jambo lililomchanganya na akashindwa kutambua chochote.
“Sawa.”
Angel alijibu huku akishusha pumzi fupi...

Siku hiyo ndiyo ilikuwa siku ya Angel kusafiri kwenda kwa shangazi yake Rebeca aishie jijini Dar es salaam.
Ilikuwa yapata saa 3:15 asubuhi ndipo Angel alianza kusindikizwa na bibi yake kuelekea stend ya mabasi ya Morogoro (Msamvu).
“Angel zingatia sana yale uliyofundwa hapa!”
Ilikuwa ni kauli ya mwisho ya babu yake pindi wanaanza kuondoka na bibi yake.
“Nitazingatia babu yangu wala usiwe na hofu.”
Alijibu Angel kisha wakayapa mgongo makaazi yale.

Usafiri wa haraka ambao ungewarahisisha kufika mapema msamvu ilikuwa ni bajaji.
Kilichofanyika hapo Bibi yake Angel na Angel walipanda bajaji ili kuwahi katika ofisi za kampuni ya mabasi alilotakiwa kusafiri nalo.
Wakafika mpaka msamvu stendi.
Waliambiwa basi la kwenda Dar es salaam lingewasiri hapo saa tano likitokea mbeya.
Angel na bibi yake walijongea kwenye mabenchi na kuungana na abiria wengine waliokuwa wakilingoja basi hilo.

Upande mwingine babu yake Angel aliwasiliana na Rebeca kwa njia ya simu kumtaarifu kuwa Angel ndiyo alikuwa anakaribia kuondoka Morogoro hivyo alitakiwa kuwahi ubungo kumpokea.
“Mtunze mjukuu wangu Rebeca nafikiri wewe mwenyewe umemwona alivyo siyo?”
“Ndiyo! Baba yuko na afya njema.”
“Sasa ole wako siku nimuone afya yake imeporomoka hatutoelewana kabisa!”
“Hapana baba hakuna kitu kama hicho!”
Rebeca alijibu, simu ikakatwa..
Maongezi yao yalikuwa yamefika tamati...

Kwingineko NGANGA ya kwenda Dar es salaam iliunguruma ndani ya stend ya Msamvu.
Abiria wote waliokuwa wakisafiri kwenda Dar es salaam waliambiwa wasimame na mizigo yao kwani mashine ndiyo ilikuwa inaingia.
“Haya haya haya wale wa kwenda Dar es salaam basi hili hapa!
Simameni na mizigo yenu kaeni mkao wa safari sasa!”

Alisikika mpiga debe akisema hivyo...
Angel alizidi kushikwa na fulaha ya ajabu sana!
Alifurahi mno hata akajikuta anatabasam bila sababu...
“Enheee! Wakati huo huo wale abiria wa kwenda Tanga, Moshi mpaka Arusha, kaeni mkao ngoma inakaribiaaaa!!”
Mpiga debe huyo alipayuka kwa mara nyingine tena!
Basi la kwenda Dar lilishapaki pale na mlango ulishafunguliwa kuruhusu abiria kuingia.
“Safari njema mjukuu wangu!”
Bibi alimwaga kwa kumpa mkono mjukuu kisha wakaachana.
Angel akapanda basi na kwenda kukaa katika siti yake maalumu iliyokuwa na namba zilizokuwa zimeandikwa nyuma ya tiketi yake.
“Abiria hakikisha unafunga mkanda kwaajili ya usalama wako.”
Kondakta wa basi hilo aliwakumbusha abiria wake kufunga mikanda kabla ya basi kuanza safari.

Ndani ya saa 5:40 basi hilo liliondoka Morogoro tayari kwa kuianza safari ya kuelekea Dar es salaam.
Katika siti aliyokuwa amekaa Angel pembeni yake alikwepo kijana mmoja ambae muda wote yeye alikuwa bize na simu yake.
Ajabu tangu Angel akae pale hata salamu hakuna yeye alikuwa bize na simu tu.
Katika vitu ambavyo Angel alikuwa hajafundwa ni kutosalimia watu.
Angel alikosa amani sana kwa kukaa na mtu zaidi ya dakika 20 na zaidi pasipo kumsalimia.
Mapajani alikuwa amepakata begi lake la nguo Angel.
Alifikiria sana ni jinsi gani angemsalimia kaka huyo lakini alikosa namna akaamua kutulia tu.
Safari ikawa inaendelea wakafika sehemu kukawa na bams/tuta Angel hakujua kama mbele kulikuwa na tuta gafla tu alishitukia gari ikidunda kwa nguvu.
Mdundo ule ukasababisha begi lake lililokuwa mapajani kutaka kudondoka.
Haraka sana akaliwahi na kulidaka kabla halijadondoka!!
Sasa bwana!
Katika harakati za kudaka begi lisidondoke chini, akamgonga huyu kaka na kifuti cha mkono!
“Hey!! Mmmh...”
Huyu kaka aligugumia kwa maumivu huku akiambatanisha na taharuki.
“Ah! Kumbe niko na mtu hapa?”
Huyu jamaa aliuliza kana kwamba alikuwa hajamuona Angel muda wote aliokuwa hapo...
“Samahani... Begi langu lilitaka kudondoka.”
Angel alijitetea.
“Hakuna tatizo mwenyewe nimeona, halafu umepandia wapi?”
Aliuliza...
“Nimepandia msamvu.”
Angel alijibu kwa utulivu...
“Daah! Nilikuwa bize na kucheza gemu hapa hata nilikuwa sijakuona aaa...
Mi naitwa Jr mwenzangu?”

“Naitwa Angel.”
“Yees! Enjo... Unaenda wapi?”
Mkaka akazidi kuchangamka...
“Naenda Dar es salaam.”
“Dar es salaam... Yes! Mwenyewe nakwenda huko kikazi, vipi wewe?”
“Mimi nakwenda kwa shangazi tu.”
“Kwa shangazi tu? Hauna mishe yoyote huko?”
Aliuliza Jr huku akifungua begi lake na kuitumbukiza smartphone yake ndani kisha akalifunga tena.
“Nakwenda kumsalimia tu!”
“Ooh! Yupo Dar sehemu gani labda?”
“Sijajua yupo sehemu gani ingawa atakuja kunipokea stend ya mabasi.”
“Oky, Kwahiyo…….!”
“Oky... Kwahiyo we Dar ni mgeni?”
“Ndiyo!”
“Ook sawa.”
Ni kama Jr aliishiwa swaga hivi akaamua kuishia hapo.
Upande mwingine Angel nae roho ilitulia kwa kuwa alishamsalimia mtu aliekuwa karibu yake basi shida yake ikawa imeishia hapo nae akauchuna!

Jr. Huyu bwana alikuwa ni kijana flani amaizing sana.
Alikuwa ni kijana aliependa utanashati wenye staha, hakuwa na ule utanashati wa kihuni hapana!
Hata mtindo wake wa kunyoa alipendelea kunyoa brash kama mwanafunzi na ndiyo staili iliyokuwa ikimtoa kuliko fashion zingine za kunyoa!
Huyu alikuwa maji ya kunde, na alipendelea kuvaa tishet nyeupee na suluari nyeusi hususan jeans.
Shingoni alikuwa akipendelea kuvaa mikufu yenye rangi ya dhahabu huku akimix na rozali jambo lililopelekea huyu fara apendeze kupitiliza.
Hivi pia ndivyo alivyokuwa amevaa siku hiyo wakati anaelekea Dar es salaam.
Jr alipoona amekwama kumuongelesha Angel, aliamua kutoa tena smart yake kubwa na foni zake kisha akaziunganisha na simu kisha kuchomeka masikioni.
Akagusa fingerprint lock ikatoka kisha akaingia sehemu ya audio na kuanza kuburudika na mziki mnene huku safari ikiendelea.

Sasa kama tunavyomjua huyu Angel siyo mzoefu sana katika safari.
Jambo lililopelekea ashikwe na uchovu ndani ya gari mwishowe alianza kusinzia!
Jr alishtukia mtu akimlalia begani.
Sasa nae kwa vile alikuwa ndani ya mziki mnene alijikuta akishituka kwa kuguswa bega na kichwa cha Angel.
Haraka akageuka...
“Oooh! Maskini mtoto anasinzia!”

Sehemu 7 Sehemu 9
0
0