Angel - Sehemu ya Ishirini na Saba (27)
“Ok sawa nitamfuata kituoni.”
Aliongea Jr huku akishika kitasa cha mlango wa gari yake…
“We mkaka wewe usiniache mwenzio ninakwenda kugeuzwa mbwa jamani.”
Maskini Angel alijisemea kimoyo moyo huku akimtizama Jr.
Machozi pia yakianza kufia taratibu kunako mboni za macho.
“Huyu dogo hii gari ni ya kwake ama?”
Mwanaume huyo nae alikuwa ndani ya maswali juu ya Jr kuhusu ile gari aliyokuwa akitarajia kuifungua…
Gafla!
Angel anaruka tiktaka moja kali na kumtandika mwanaume yule mateke mawili dabo.
Moja likitua sehemu za siri na lingine likitua eneo la kitovu...
“Aaaaaagh!!”
Yule mwanaume alipiga ukunga mkali wa maumivu huku akijitahidi kujikaza lakini wap…!
Maumivu yalikuwa ni makali mno kitendo kilichopelekea ajikunje.
Wakati Angel akiwa anapepesuka pepesuka ajiweke sawa...
Jr nae huyo!
Akaja na sarakasi moja matata sana ambayo teke lake lilikwenda kumpata mwanaume huyo kisogoni mpaka akenda kuisalimu ardhi…
Na bastola kule...
“Angel kimbia njoo polisi wanakujaaa!”
Jr alikimbia na kwenda kumshika Angel mkono na kumvutia kwenye gari ili watimke maana nyuma yao vilisikika ving'ora vya gari za polisi.
“Funga mkanda! Funga mkanda.”
Jr alimhimiza Angel kufunga mkanda wakati huo akiiondoa cruza yake kwa mwendo wa aina yake.
Dakika moja baadae Rebeca anatimba eneo la tukio akiwa na gari mbili za polisi...
Anamkuta mtu wake akiwa kakaa chini huku akiwa ameshikiria sehemu zake za siri...
“Sadiki nini tena?”
Kumbe huyu mwehu anaitwa Sadiki...
“Nimepigwa na huyo dada keshaondoka!”
Aah!
Rebeca alipaniki vibaya mno.
“We nae mwanaume gani bwana? Unapigwa na mtoto wa kike…
Unaniaibisha Sadiki.”
“Ungeuliza kwanza nini kimetokea?
Alikuwa na nani…
Sasa unavyoanza kupaniki unajua nini kimetokea?
Kuwa mtaratibu basi.”
Sadiki akamtuliza Rebeca namna hiyo.
Rebeca kusikia hivyo akatulia, hata yeye alitambua kuwa alikosea!
Hakupaswa kupaniki kiasi hicho pasipo kujua sababu juu ya kile kilichokuwa kimetokea.
“Sorry… Sasa imekuwaje tena mtu wangu?”
“Hapa nimewakuta wapo wawili tena wana gari, sasa nilipojaribu kukaweka chini ya ulinzi hako kadada yule mwenzake
ambae ni kijana alikuja juu, nilipojaribu kumtuliza wakanichangia.”
Maneno ya Sadiki hayo, mpelelezi wa Rebeca…
“Oooh! Shiiiit…
Sasa wameelekea wapi?
Na wana gari gani?”
Akauliza Rebeca huku akikosa amani kabisa.
“Wameenda na barabara hii hii na wapo na gari aina ya Toyota land cruiser.”
Daah!
Rebeca alichanganyikiwa mno!
“Brother hukuweza kukariri namba za gari yenyewe?”
Askari aliuliza...
“Hapana! Kwa sababu waliniacha nikiwa nimeanguka vibaya na wao waliondoka kwa kasi.”
Sadiki alijitetea hivyo lakini ukweli ni kwamba hata hakukumbuka kuangalia namba ya gari hiyo kutokana na maumivu
makali aliyokuwa akiyasikilizia wakati huo.
Chezea maumivu ya dushelele?
Huko siyo bwana!
“Kwahiyo mama inakuwaje hapa?”
Askari polisi mmoja alimgeukia Rebeca.
“Hatakiwi kuondoka kabisa ndani ya ndani ya Dar es salaam, fanyeni juu chini wakamatwe kumbe wapo wengi hivi?”
Huwezi kuamini.
Kisa pesa tu Rebeca amebadilika utafikili Angel siyo ndugu yake.
Wakati ni mtoto wa kaka yake kabisa tumbo moja, nyonya ninyonye lakini kwa kuwa Angel alimkatalia kuuza Bikra yake
kwa tajiri mfanya biashara John kwa dau la shilingi milioni thelathini, basi hiyo ndiyo sababu ya kumkatili kiasi hicho mtoto
wa mwanamke mwenzi.
Basi kwa kuwa Rebeca kaamuru polisi watasema nini tena?
Difenda zikaingia barabarani...
“Wiu! wiu! Wiu! Wiu! Wiu! Wiu! Wiu! Wiu! Wiu!”
Zilikuwa ni sauti za ving'ora vya magari ya polisi wakati wanamfuatilia Angel...
Spidi waliyokuwa nayo haikuwa na mfano!
Pwani waliingia muda huo huo na sasa walianza kuitafuta Tanga...
Unaweza pia kusoma: