Dunia Ya Pili - 10
Kilikuwa ni kitendo cha aibu sana kwangu hasa kwa waliokuwa wakinitizama kwani nilionekana ni mdada wa heshima na mwenye pesa zake sasa iweje
nitekwe na mtu wa ovyo kama yule anukae kikwapa, bangi na pombe zingine za ajabuajabu?
Hakika ilikuwa ni aibu kubwa sana, aibu ambayo kwa wakati ule sikuiona wala kuihisi sababu ya pombe nyingi nilizokuwa nimekunywa nikalewa chakali.
Mara ya pili licha ya kuhisi msisimko wa aina yake mwilini mwangu, nilijitahidi nikautoa mkono wake lakini alivyorazimisha na kunipapasa kwa mara ya tatu…
Nilipagawa, nikashindwa kujitetea nikajikuta natulia tuli.
Yule kijana akaona hiyo ndiyo nafasi kwake, alinipapasa kwa spidi ya kushangaza ghafla nikashitukia kafika kifuani.
Matiti yalichambuliwa kama nyanya saa hiyo nikihisi nywele nazo zikiupokea kwa ufasaha kabisa msisimko mwingi uliotoka kwenye matiti yangu,
nikazidi kudata hisia za ngono zikanijaa nikatamani hata tuondoke muda huohuo.
Ghafla nikahisi harufu kali ya bangi ikipita kwenye matundu ya pua zangu nilishituka nikakaza macho nione hii harufu inatoka wapi?
Kufumbua nakutana na mdomo wa yule kijana ukiukaribia mdomo wangu, nilishtuka nikarudisha kichwa nyuma.
“Mmh!”
Niliguna.
“Vipi mrembo?”
Aliuliza.
Sauti yake ilitoka na harufu kali ya bangi na pombe mchanganyiko, ilikuwa ni harufu mbaya sana iliyonikata mpaka stimu za ngono zilizokuwa zimeniandama.
“Hapana niachie.”
Niliongea huku nikimsukuma atoke nae akaning’ang’ania.
“Tuliiaaa basiiii.”
“Tokaaaa!”
Niliwaka kama mbogo jike mwenye ndama, hata nikajaribu kumsumkuma kwa mara ya pili lakini alining’ang’ania kwa nguvu.
Nikamsukuma kwa nguvu mara tatu huku nikitumia nguvu maradufu hata mkono wake mmoja ukamponyoka alipepesuka huku akiwa kanishikilia kwa mkono mmoja
ghafla akaingiza mkono mfukoni akatoa sindano yenye kumiminika ndani bahati nzuri niliiona mapema nikapiga kelele kwa nguvu.
“Ananibakaaaaaaaaaa!!”
Nilimsukuma kwa nguvu hadi akaniachia akayumba na kwenda kuanguka.
Mara Farid alitokea hata nisijue alitokea wapi?
Ndiye alikuwa mtu wa kwanza kufika mahali nilipokuwepo ndipo na wengine waliokuwemo ndani ya bar ile wakafurumka kama nyuki kuja kwangu.
Farid alivyofika tu alimvaa yule mlevi na kuanza kumshushia kipigo kitakatifu.
Ghafla Farid nae alipiga ukunga.
“Ana kisuuuuuu, jamani kisuuuuuu!”
Alipiga kelele mara mbili huku akimwachia bahati mbaya yule mlevi walishindwa kumdhibiti baada ya watu kusikia ana kisu wakasita kumsogelea
hadi akakurupuka na kukimbia huku akimwacha Farid akiwa amesimama huku anayumba kama mlevi aliezidiwa pombe.
Watu wengine wakamuungia kumfukuzia lakini hawakuweza kumkamata hata sikujua alifanikiwaje kukimbia katika eneo lile lenye mkusanyiko wa watu wengi.
Haraka nilimsogelea Farid.
“Farid vipi uko salama?”
Nilimuuliza huku nikimtizama kila kona ya mwili wake.
“Niangalie nimechomwa na kitu chenye ncha kali ubavuni.”
Alijibu huku akifungua shati lake.
Alivyovua shati saa hiyo na watu wengine wakawa wamesogea alionesha sehemu alipochomwa, kilikuwa ni kijeraha kidogo sana cha sindano bila shaka sindano
ile niliyoiona kwa mlevi yule ndiyo aliyochomwa nayo Farid.
“Usiwaze Farid ni kajeraha kadogo sana utapona usijali.”
“Naishiwa nguvu.”
Aliongea huku akizidi kuyumba mwisho alijiachia, lakini watu walimwahi na kumdaka ili asiangukie viti vya bar.
“Farid…”
Hakika kilikuwa ni kitendo cha kushangaza mno, hali ilizidi kuwa mbaya kwa kijana yule taarifa zilisambaa muda huohuo wenzake walifika na kumchukua
kwaajili ya kumkimbiza hospitali.
“Poleni sana chukueni hii itawasaidia huko mbeleni.”
Nilitoa kiasi cha shilingi elfu hamsini nikawakabidhi wale vijana waliokuwa katika harakati za kumkimbiza Farid hospital.
Hatimae waliondoka zao.
“Dada usiwe unapendelea kukaa peke yako ujapo bar kaa karibu na watu kuna vijana siyo wazuri kabisa.”
Aliongea mhudumu mmoja aliepita karibu yangu.
“Sawa asante kwa taarifa.”
Hata hivyo sikuona tena sababu ya kuendelea kukaa hapo hivyo niliondoka muda huohuo kwani tayari ilishakuwa mchana.
Nilitoka nje nikaiona Mwangata yote ikitembea, yote hii ni kwa sababu ya pombe nyingi nilizokunywa.
Kutokana na jua lilivyokuwa kali mchana ule nilishindwa kuendelea na safari sababu ya pombe ilibidi nirudi tu bar huko nilichukua chumba nikaenda
kujipumzisha ili pombe ipungue ndipo niendelee na mambo mengine.
Nikiwa chumbani huko nimelala nilipitiwa na usingizi mzito kisha niliota ndoto moja nikiwa na Amina sehemu moja isiyofahamika halafu tulikuwa tunaongea.
“Pole wifi… Lakini una matatizo makubwa sana kwenye maisha yako.”
Yalikuwa maneno ya Amina.
“Kwanini wifi?”
Nilimuuliza.
“Umeingia kwenye mikono ya agano baya sana, agano ambalo limekula vizazi vyenu karibu vyote hata wewe wanampango wa kukuchukua ufanane nao lengo kubwa ni
kuja kuuteka ukoo wenu wote hata walio mikoa mbalimbali, lakini pia viumbe hao wanampango wa kuiteka Iringa na viunga vyake vyote na hata nchi nzima
baadae viumbe hao wataleta maafa hata kwa dunia.”
Alisema.
“Kivipi?”
“Viumbe hao wenye uhusiano wa karibu na fremaason ya Lucifer wanampango wa kujiimarisha zaidi pia wanampango wa kutengeneza kirusi chenye asili ya kirusi
cha zombi isipokuwa kirusi chao hakitaweza kuudhuru mwili wa binadamu kwa kuuharibu bali kitaudhuru kwa njia nyingine tofauti kabisa.”
“Kirusi?”
“Ndiyo!… Je wajua kuwa wanakuwinda sana? Kuna sindano ya sumu yenye kirusi cha kuhamasisha ngono lengo ni uchomwe sindano hiyo ukishachomwa basi
utakuwa ni Malaya uliyekubuhu utafanya ngono na kila mwanaume atakayetokea mbele yako pia utakuwa ni chanzo cha kusambaza kirusi hicho kwa watu wengi
na hiyo itakuwa ni hatua ya kwanza… Tatizo likishakuwa kubwa wao watatoa mtaalamu atakaekuja na dawa za kutibu tatizo hilo ambapo mtaalam huyo atakuwa na
sindano zingine tena zenye kirusi kingine kipya chenye athari kubwa sana kwa mwanadamu, kirusi hiki kinaweza kuwa hatari zaidi ya kirusi cha zombi.”
Maneno Amina yaliniacha kinywa wazi siyo kawaida, ilikuwa ni ndoto ndefu sana Amina aliliongelea kwa upana sana swala lile mwisho aliniambia ili niepukane
na jaribu hili ilinipasa nikimbilie makanisani, kwani yeye huniombea mimi sana ndiyo maana malaika akampa uwezo wa kukutana nami kupitia ndoto.
Usingizi ulipoisha nilikupurupuka kama mwehu huku moyo ukiniendea puta sana.
“Nini hiki?”
Nilijiuliza.
Muda huohuo nikalikumbuka tukio lililotokea mchana ule pale bar, nilimkumbuka mtu aliekuja kama mhuni tu wa mtaani alielewa pombe lakini kumbe
haikuwa hivyo mtu yule alikuwa na hila kwangu.
“Yule ni nani na katokea wapi?”
Nilijiuliza saa hiyo nikimkumbuka na yule wa Miami aliyekunywa pombe aliyotia kumiminika ambacho nilitakiwa ninywe mimi baadala yake alikunywa yeye na alifariki.
“Kwahiyo ningekunywa mimi nisingekufa?… Mmh haya mambo mbona siyaelewi?”
Nilijiuliza saa hiyo nikishuka kitandani.
Niliingia bafuni nikajimwagia maji kuondoa jasho kisha nilirudi chumbani huko nilivaa nguo zangu nikavaa na mkoba wangu nikatoka, tayari pombe zilikuwa
zimepungua kwa kiasi cha kutosha.
Wakati huo ikiwa yapata saa kumi na robo arasili, kiufupi tayari ilishakuwa jioni.
Nilitoka nikatembea mpaka stendi ya kidamali hapo nilipanda moja kati ya daladala zilizokuwa zikielekea Ipamba.
Nayo haikuchukua muda daladala hiyo iliondoka stendi kupisha foleni ya wenzie baada ya muda wake kuisha.
Daladala hiyo iliingia barabarani, licha ya kuwepo kwa vituo vingi barabarani niliwahi kushuka njia panda ya Kalenga bado mapema tu.
Hapo nilichukua bodaboda iliyonikimbiza mpaka karibu kabisa na nyumbani, sikutaka dereva bodaboda huyo anifikishe kabisa nyumbani ndiyo maana nilimwambia
anishushie nyuma kidogo.
“Nidiyo hapa?… Dada si nikufikishe nyumbani tu?”
“Wala usijali nimeshafika kuwa na amani tu.”
Nilimjibu hivyo saa hiyo nikimlipa ujira wake.
“Mmh! Dada hii chenji changamoto.”
Aliongea hivyo baada ya mimi kutoa noti ya shilingi elfu kumi.
“Usijali utanywea chai cheji itakayobaki hapo.”
Nilimwambia akaniangalia mara mbili asiamini alichokisikia.
“Asante sana dada angu mwenyezi Mungu akuzidishie sana.”
Sikumjibu baadala yake nilitoa simu yangu nikawa bize hadi akaondoka.
Nilikagua bastola na kisu kama vipo, niliviona vimetulia kama vilivyowekwa sambamba na burungutu la pesa.
Nilifunga vyema zipu ya mkoba wangu kisha nilimpigia Amina simu.
“Uko wapi wifi?”
Nilimuuliza baada ya simu kupokelewa.
“Nipo nyumbani wifi yangu wewe upo wapi?”
Aliuliza.
“Nipo mtaa wa pili hapa.”
“Upo na baba?”
“Baba?”
“Ndiyo… Alikuja kukufata baada ya kusikia unaachiliwaa na hauna hatia yoyote.”
“Hata sijaonana nae, shangazi yeye je? Hakufika hapo?”
“Waliwasiliana na baba kupitia simu walikuwa wakijadili kuhusu wewe sasa sijajua kama watakuwa wameenda wote mjini au laa.”
“Haya sawa… Njoo basi unipokee.”
“Sawa wifi nakuja.”
Nilikata simu wakati huo akili yangu ikiwa kwenye tranka nilipolihifadhi jiwe kubwa la dhahabu, sikuwaza chochote kuhusu Meddy sikuwaza chochote
kuhusu mwanangu na sikuwaza chochote kuhusu ndugu zangu kiufupi akili yangu ilihamia moja kwa moja kwenye pesa na starehe tu.
Unaweza pia kusoma: