Dunia Ya Pili - 09
Nilibaki nimeduwaa mfano wa mwizi aliyefumaniwa akiiba!
“Chini ya ulinzi!”
Ilisikika sauti moja ngumu ya kiume ikiniamuru.
Nilitizama kitandani nikaona bastola niliyotoka nayo Miami bar, nikaimezea mate lakini kwa muda huo sikuwa na uwezo wa kuikota tena kwanza hata kuitumia
nilikuwa sijui zaidi ya kukariri tu.
“Tunaondoka na wewe gari ipo nje hapo.”
“Siwezi kuondoka, kwanza ninyi ni kina nani?”
Niliuliza.
“Majibu yako utayakuta kituoni, tuondoke.”
Mwanaume alienijibu hivyo alinisogelea kabisa akanishika akataka kunikokota tutoke nje, nikamgomea na kujinasua kwake kinguvu.
“Paaaaah!”
Nilipigwa kofi zito, nikakurupuka kitandani!
Dah! Kumbe ilikuwa ndoto!
Nilichoka.
Kwanza niliamka nikaketi, saa hiyo moyo ulikuwa unaenda mwendo wa hali ya juu hata nikashusha pumzi nzito.
“Nini hiki?”
Nilijiuliza saa hiyo nikinyoosha mkono nikaokota simu yangu.
Nilitoa loki nikatizama saa ikaniambia saa hiyo ni saa saba na robo usiku.
“Mmh kumbe muda umeenda, inamaana kumbe nililala muda uleule hadi nimeota?”
Niliongea nafsini wakati huo nilitoa earplane mode simu yangu niliiweka pembeni nikalala kujaribu kutafuta usingizi tena.
Lakini mawazo hayakubanduka tena kichwani,ile ndoto iliniharibia saikolojia yangu kichwani, sikutaka kuamini moja kwa moja kwamba ile ilikuwa ni ndoto tu?
Mawazo ya kwamba ndoto ile ilikuwa na ujumbe fulani yakaniandama.
“Hii siyo bure, ikumbukwe sasa hivi tayari nimekwisha tenda matukio mawili ya mauaji hivyo kutafutwa lazima.”
Nilijiambia nafsini.
Basi kwanzia muda huo sikuweza kulala tena usingizi, nilijigeuza geuza kitandani nikalala kila staili kwa lengo la kutafuta usingizi lakini wapi, usingizi ulipaa kabisa!
Mpaka majogoo yanakuja kuwika mimi nilikuwa macho.
Mawazo ya kukamatwa na polisi yakazidi kunitesa kichwani amani nikakosa nikawa mtu mnyonge na mwenye mawazo tele.
Ilipotimu saa kumi na mbili simu yangu iliita, nayo pia ilinipa mashaka.
Niliichukua na kuitizama nikaona mpigaji ni Sam.
“Hallo.”
Nilipokea.
“Mambo Leylah.”
“Safi vipi?”
“Poa umeamkaje?”
“Nimeamka salama kabisa… uko wapi?”
Aliuliza nikakosa jibu sababu ninachojua Sam yupo uko kwenye dunia yao sasa ananiuliza niko wapi je? Sehemu za mji wangu anazifahamu?
“Mimi nipo mitaa ya posta naelekea kituo kikuu cha polisi Iringa we upo wapi?
Aliuliza tena kwa mara ya pili moyo ukalipuka puuh!
Neno ‘Kituo cha polisi’ lilinipa kiwewe moyoni.
“Nipo Mlandege.”
Nilijibu japo kwa kujilazimisha.
“Kuwa huru Leylah, leo uchunguzi unakamilika na utakuwa huru kuanzia saa mbili asubuhi.”
Aliongea Sam.
“Kivipi?”
Nilihoji kwa shauku kubwa sana!
“Niamini mimi.”
Sam alikata simu.
Nikabaki nimeshikilia kifua changu, kuna chembe fulani ya furaha ilinijia nikawaza jinsi nitakavyokuwa na maisha mazuri nikiwa na pesa halafu
nina amani, sina stress wala mashaka na chochote.
Papo hapo nilikumbuka kitu, haraka nikampigia Sam simu.
Iliita mara moja tu ikapokelewa.
“Hallo… We hiyo ni mali yako halali yule alilala usingizi wa milele, ile sumu aliyotaka kukunywesha wewe ukamshtukia alivyokunywa yeye alifariki…
Huyo ndiyo tabia zake mashariti yake ya mali yalimtaka kuua sana wanawake ndiyo maana alikuwa akiua kwa staili hiyo ndiyo maana nae jana zamu yake ikamkuta.”
Moyo ulipiga mkambo wa nguvu, kwanza nilijiuliza Sam alijuaje hali ya kuwa sikuwa nimemwambia japo nilimpigia kwa lengo la kumhabarisha kuhusu hicho
kilichotokea na hii bastola niliyoondoka nayo.
“Umejuaje Sam?”
Nilijikuta nimelopokwa na swali lile ambalo hata sikutegemea kuliuliza.
“Si nilikwambia ulimwengu wetu haujawahi kufichwa na siri… Hivyo usiumize kichwa kuhusu mimi we cha kufanya chukua kila kitu uje nacho nitakapokuita.”
“Sawa.”
Nilijibu.
Simu ilipokata niliwaza sana, haya maisha niliyoingia ni maisha gani? Na kwanini kila siku yanakuja mapya?
Nilijiuliza bila kulipata jibu.
Nikaichukua bastola ile nikaitizama vizuri, ilikuwa ni bastola nzuri mno nyeusi aina ya Colt 7 baada ya kuisabahi nikaiweka kando nikaokota mkoba
wangu nikamwaga kitandani vitu vyote vilivyokuwa ndani ya mkoba, nikachukua kitambulisho na kukitizama kwa makini nikakisoma kwa makini, nikagundua yule
mwanaume alikuwa injinia mkuu wa TANROAD Iringa.
Napo nilishituka! Nikajiuliza hii nayo haiwezi kuwa balaa?
Muda huohuo nilichukua simu yangu na kumpigia Sam.
“Leylah.”
Alipokea kwa kulitaja jina langu.
“Hivi we Sam mbona yule mtu kitambulisho chake kinaonesha ni injinia mkubwa tu serikalini? Hii haiwezi kuwa shida nayo?”
“Hicho ni kitambulisho batili, kama huamini soma jina la kitambulisho pia soma jina kwenye kadi zake za benki.”
Nilivyosikia hivyo haraka nilichukua kadi ya CRDB nikasoma jina nikatabasamu, nikachukua kadi ya NMB, nikasoma jina nikashangaa.
“Mbona kila kadi na jina lake? Kwamba hazikuwa zake?”
Nilimuuliza Sam kwani simu haikuwa imekatwa.
“Huyo ni tapeli na jambazi anaetumia ushirikina kutafuta pesa kama nilivyokuwa nimekuelezea awali kuhusu yeye na wanawake potezea
kuhusu yeye na hakuna chochote kitakachotokea kwani hata mhudumu wa vyumba aliekuhudumia jana alifariki usiku kwa ajali ya bodaboda wakati
akiwa njiani anaenda kwa mwanaume na ni yeye pekee ndiye aliefahamu kuwa wewe ulichukua chumba pale, kwahiyo hapo ni amani kama mbinguni.”
Maneno ya Sam yaliniacha na mshangao uliochanganyika na furaha kuu ndani yake, niliziangalia pesa nyingi zilizokuwa pembeni ya kitanda nilichokuwa
nimelalia hakika nilijikuta mwili mzima unasisimka kwa furaha.
Basi baada ya simu kukata, nilisimama nikaingia msalani kumwaga maji.
Baada ya kutoka huko niliingia bafuni nikajimwagia maji, nikapiga mswaki kisha nikatoka na kurudi chumbani huko nilibadilika nikajiweka
sawa vitu vyote kuanzia bastola, pesa, kadi za benki pamoja na kile kitambulisho nikavirudisha kwenye mkoba, nikaubeba kisha simu niliishika mkononi
nikatoka zangu na kukabidhi chumba kisha niliondoka zangu.
Ilikuwa yapata saa moja na nusu asubuhi, hali ya hewa siku hii ilikuwa baridi mno nyakati zile za asubuhi katika ukanda wote wa nyanda za juu kusini
sababu ya hali ya mawingu iliyokuwepo.
Baada ya kutoka Serengeti niliikamata barabara ya kutokea Check-point nilivyofika mitaa ya Check-point nikaikamata barabara iliyoelekea kulia
kwangu, hiyo ikanifikisha moja kwa moja mpaka mitaa ya mwisho wa lami.
Sehemu hii ina migahawa mingi iliyojengwa kwa mbao, kutokana na hali ya hewa ilivyokuwa asubuhi ile nilishawishika kuingia mgahawani ili nipate chai.
“Karibu dada.”
Kijana mdogo wa kiume ambae alikuwa ni kijakazi katika mgahawa nilioingia alinikaribisha kwa heshima.
“Asante… Chai ya maziwa ipo?”
Niliuliza.
“Ndiyo, pia vitafunwa vipo tayari. Kuna mikate, maandazi, chapati, sambusa na kiporo cha wali.”
“Sawa niletee chai ya maziwa na mikate miwili.”
Nilichagua kula mikate sababu nilikuwa nahisi njaa pia.
Nilihudumiwa kama nilivyohitaji, nikapata chai hadi nikahisi sasa tumbo limekuwa zito, pia mwili nao ukachangamka kwa sababu ya chai ile ya
moto nikalipa na kuondoka.
Kitendo cha kutoka nje ya mgahawa tu simu yangu iliita.
Kuangalia nikagundua mpigaji ni shangazi.
“Hallo!”
Nilipokea bila hata kujali chochote.
“Upo wapi Leylah?”
Niliuliza, lakini kuna kitu kilinishitua.
Sauti yake ilikuwa ya upole mno! Kwanza nikaganda nisijue nimjibu nini?.
“Rudi nyumbani Leylah, wakwe zako wanalia wanataka wakuone wakuombe msamaha kwa kile walichowaza juu yako Leylah.”
“Haaaa! Nirudi kufanyaje wakati mnanituhumu kuwa mimi ni muuaji nimemuua ndugu yenu?”
Nikajikuta nimebwatuka kwa sauti ya juu hata bodaboda na watu wengine waliokuwepo karibu wakanitizama kwa mshangao.
Nikajishitukia.
“Siyo hivyo Leylah wewe rudi kwanza.”
Nilikosa jibu, nikashusha pumzi nikahisi hasira kwa mbali lakini tena nafsi ikanisuta.
Shangazi alikata simu baada ya kuona siongei.
Ile anakata tu simu ya Amina nayo iliingia.
“Mmh! Hawa watu vipi?”
Nilijiuliza huku nikipokea simu ile.
“Hallo!”
“Wifi?”
Aliniita.
“Niambie.”
“Uko wapi wifi yangu?”
“Kwanini unaniuliza… Unataka kuja kunikamata?”
“Siyo hivyo wifi tusamehe sana… Nafsi na fikra zetu zilitenda zambi juu yako tusamehe wifi tunaomba urudi nyumbani tunasikia umeachiliwa kituoni.”
Neno “Tunasikia umeachiliwa kituoni” nalo lilinistaajabisha.
“Sawa nitakuja.”
Nilijibu kifupi lengo akate simu ili nimpigie Sam kuna kiu nilikumbuka Amina alipotaja neno “Kituoni”.
“Lini?”
“Kata simu kwanza nitakupigia.”
Alivyokata nilimpigia Sam.
“Leylah.”
“Abee.”
“Bado umelala?”
“Hapana.”
“Kuna simu umepigiwa tangu imetimu saa mbili?”
“Ndiyo nimepigiwa nyumbani lakini sijaelewa vizuri ndiyo maana nimekupigia.”
“Ahaa! OK ipo hivi… Uchunguzi umebaini kuwapo haukuhusika katika kifo cha mumeo kama ilivyodhaniwa na wengi bali mumeo alikuwa na bifu na mtu fulani
aliemhisi kuwa anatembea na mke wake na ndiye aliefika kwenu kutekeleza unyama huo, alama za vidole katika kisu vilibainisha na mtu huyo anafahamika
vyema kabisa isipokuwa hajulikani alipo tangu atekeleze tukio hilo.”
Maelezo yale yaliniacha na mshangao wa ajabu, kweli ukistaajabu ya musa basi ya firauni utayaona.
Pia Sam aliniambia alikuwa anahitaji kuonana na mimi.
“Sasa tutakutana wapi?”
Nilimuuliza.
“Utanikuta garden pale posta.”
Alijibu.
“Sawa.”
Nilimjibu kisha muda huohuo nilikwea bajaj iliyonikimbiza moja kwa moja mpaka kituo chao cha mashine tatu hapo nilishuka nikaanza kutembea
mdogomdogo kuelekea post, palikuwa mbali kidogo nilihitaji tu kufanya mazoezi.
Nilitembea mpaka nafikia stendi ya zamani, Sam alipiga simu tena.
“Nipo stendi ya zamani hapa.”
“Sawa.”
Nilitembea hadi nikafika, kweli nilimkuta Sam akiwa galden ananisubili.
“Karibu Leylah.”
Sam alinikaribisha kwenye kiti cha kulipia ambacho bila shaka alikuwa amekwisha kilipia.
“Asante.”
Niliketi pale bila kupoteza muda Sam alieleza alichoniitia haswa, aliniambia sasa naelekea bilionea wa kuogopeka kwani mambo yote yalishakaa
sawa akaniambia kuwa nilitakiwa kwenda nyumbani kwa wakwe nikalichukue lile jiwe la dhahabu lenye thamani ya shilingi za kitanzania Bilioni sita
na marupurupu kisha tungekwenda wote kuliuza Afrika kusini halafu ningerudi huko nikiwa na pesa nyingi sana pesa ambazo hata ningekaa bila kufanya
kazi maisha yangu yote na nikafanya kila aina ya starehe bado zisingeisha.
Nilishangaa!
Pia akaniambia ile nyumba niliyonunua haikuwa na hadhi kabisa nilitakiwa kuivunja ili nijenge nyumba ya kifahari ambayo huenda ingekuwa tishio mji mzima.
“Sawa nimekuelewa, lakini Sam kwani wewe unafanya kazi katika kituo kikuu cha polisi cha mkoa ama?”
Nilimuuliza ni swali lililokuwa linanipwelepweta sana.
“Hahahahaha!… Swali zuri lakini mimi sifanyi kazi katika wizara yoyote ya serikali ya Tanzania isipokuwa nina uwezo na ujuzi wa kuingia sehemu
yoyote kwa maandishi na vitambulisho vyote ninavyotakiwa kuwa navyo mahali hapo, mfano nimekuja kituo kikuu cha polisi cha mkoa nikiwa kama askari mpelelezi
wa kujitolea kutoka serikalini nikaja na viambatanishi vyote vilivyokuwa na uwezo wa kuniruhusu kushughulikia kesi yako, nilipokelewa na swala nimelimaliza.”
Kwa maelezo yale niliishia tu kumtizama Sam hata nisijue niongee nini tena?
Uwezo wake uliniachia tafakari ya aina yake.
Tuliongea mengi mwisho alidai kitambulisho na kadi za benki nilizokuwa nazo, nilimpa baadae tuliagana, akanisisitiza nifike nyumbani
nikachukue lile jiwe la dhahabu ili tupange utaratibu wa kulisafirisha.
Baada ya hapo tuliagana tukaachana, sasa nikaanza kupiga hesabu za kurudi nyumbani Kalenga sababu ndipo tunapoishi na nikaolewa hapohapo.
Muda mzuri niliona ni jioni.
Mchana huo nikaona nitafute sehemu nitulie nianze kupanga mikakati yangu kichwani ya kimaisha.
Nilitoka garden nikaingia barabara kuu, nayo nikaiambaza mpaka TANESCO mbele kidogo nikachepuka na kuingia maduka ya Miyomboni.
Kitendo cha kufika Miyomboni nikakumbuka kitu.
Muda huohuo niliingiwa na akili fulani ya kikatili nikanyooka moja kwa mpaka mahali niliponunua mkoba siku iliyopita bahati nzuri yule
alieniuzia mkoba siku iliyopita sikumkuta.
Nilimkuta tu mama mwingine wa makamo ndiye kaketi dukani.
Nilimsalimia, baada ya salamu nilimuuliza kuwa muuzaji wa siku zote yupo?
Jibu lilikuja kuwa aliacha kazi siku iliyopita ndiyo maana kaamua auze yeye kwa hizi siku mbili tatu wakati akiwa anafanya utaratibu wa
kumpata mwingine.
Nikagundua kanikimbia mimi huyo.
Basi nikamwambia tu yule mama kuwa huyo ndo nilikuwa na shida nae kama hakuwepo basi.
Niliaga nikaondoka, hapo nilikuwa nimechoka kutembea nilisogea kituo cha bajaj hapo Miyomboni nikapanda Bajaj iliyonipeleka moja kwa moja hadi Mwangata.
Nilishuka Mwangata stendi ya Kidamali hapo nilitafuta bar nzuri nikaenda kujichimbia huko.
Bar hii sikuisoma jina lake ingawa ilikuwa ni nzuri mno na ilikuwa na vyumba vya kulala pia.
Nikiwa mle nilitafuta kiti cha peke yangu nikaenda kuketi huko nikatulia kimya.
Punde si punde mhudumu alifika kunisikiliza.
“Niletee chupa kubwa ya wine na Grand Malta kubwa mbili.”
Mhudumu aliondoka baadae alirudi na vinywaji nilivyomwagiza, alinifungulia wine akaimiminia kwenye glasi kisha nami nilichanganya na
Grand Malta nikaanza kunywa taratibu.
Nilikunywa taratibu wine yangu huku nikiperuzi mtandaoni na simu yangu janja mwisho nilihisi kulewa, nilichokifanya nilitoka nje nikaagiza supu ya ng’ombe.
Nilirudi nikaendelea kunywa, mara supu ilifika ikiwa na kila aina ya viungo, nilipata supu ile huku nikifurahi radha murua ya supu hiyo iliyopikwa kwa
ujuzi wa hali ya juu.
Baada ya supu niliendelea kunywa, nilikunywa mwisho nilijisahau nikanywa nikazidisha pombe nikalewa.
Baadae kuna kijana mhuni tu wa mtaani asiye na hadhi yoyote alikuja na chupa ya bingwa mkononi.
“Dadaa vipiiii?”
Alinisamia kilevi mno! Alionekana wazi alikuwa amelewa mno,huenda alikunywa kwanza pombe za kienyeji huko vilabuni kisha akaja kusumbua bar na chupa ya bingwa.
“Kunywa pombe wewee unakunywaaa pombeee ganiii hiyoo? Kunywaa hiii.”
Nami nilimsapoti kwa kuwa nami nilikuwa nimelewa chakali nikamkaribisha akamalizia wine iliyokuwa imesalia.
Kijana akawaeuka, mashetani ya ngono yakampanda na jinsi pombe zisivyo na adabu alianza kunilopokea maneno ya kunitaka kimapenzi.
“Ujuee niniiiiiiiii… Sistaaa wewe ni mrembo kinyamaaaa… Nakupenda sanaa!”
Aliongea huku akileta mkono wake na kuanza kunipapasa mapaja, mwanzo niliutoa mkono wake lakini aliporazimisha na kunipapasa mara ya pili nami nilihisi
msisimko wa ajabu mwilini nikatamani lile zoezi liendelee…
Unaweza pia kusoma: