Hello! Karibu HASCAVELA

Muonekano wa Giza:

Msaada

Dunia Ya Pili - 22

“Usinue tafadhari nipo chini ya miguu yako.”
Aliongea Abdalah Kizau huku akiwa ni mwenye uwoga wa hali ya juu, tayari mikono yake ilikuwa juu mwili mzima ukiwa umemtapakaa mapovu.
“Kwanini ni msaliti?”
Nilimuuliza huku nikiwa makini nae nikihofia asije akanipora silaha akanigeuka.
“Wewe ni nani? Lakini usinue samahani lakini nina mwanangu bado mdogo mke wangu ananitegemea.”
Alianza kulia.
“Mke wako yuko wapi?”
“Yupo Marangu.”
“Na wewe huku unafanyaje?… Unamsaliti siyo?”
“Jestina amekutuma uniue? Usifanye hivyo nitakupa pesa tafadhari.”
Nilimwangalia kwanza nikamzarau kabisa.
“Hata siyo Jestina… Ila kosa lako ni moja tu, imejiunga na jumuiya ya siri halafu ukaisaliti, mbaya zaidi ukatoa siri ambazo hukutakiwa hata kufungua kinywa chako ukatamka sentesi hata moja!
Wewe ukafanya hivyo kwa kujifanya umeokoka!
Na sisi hatujawahi kuvumilia upuuzi kama huu… Tangulia kuzimu Abdalah Kizau.”

Pale pale nilimfyatulia risasi ambazo zote zilimpata katikati ya paji lake la uso kichwa kikafumuka hata ubongo ukamwagika nje!
Akaanguka chini kwa kishindo kama gunia la mtama puuuh!
Mi nikaondoka zangu nilipita mpaka ukumbini, nikaona kila mtu anashughulika na mambo yake hakuna hata mmoja alienitizama mpaka natoka kwenye Bar hiyo.

Ilikuwa yapata saa mbili na dakika nane usiku…
Nilivyoshuka ghorofani na kutoka nje, nilitembea mpaka maeneo ya soko la mlandege hapo nilitafuta sehemu tulivu nikatoa simu yangu nikampigia Sam.
“Leylah…”
Alipokea simu kwa kuniita jina langu.
“Abee mume wangu.”
“Vipi?”
“Safi niambie.”
“Safu tu.. Uko wapi?”
“Geto apa.”
“Mmh! Umelala?”
“Walaa… nipo nabadilika hapa si unajua baada ya kazi?”
“Sawa kwahiyo unakuja Mlandege?”
“Ndiyo we uko wapi kwani?”
“Utanikuta Chek point.”
“Sawa.”
“Sam fanya hivyo bwana nimekumbuka kitu kutoka kwako.”
“Usiwaze!”
“Poa.”

Nilikata simu baada ya maongezi, palepale nilichukua bodaboda iliyonikimbiza mpaka Chek point huko nilienda kuonana moja kwa moja na mhudumu wa vyumba nikachukua chumba na kuingia nikajifungia.
Muda huo sikujisikia kunywa pombe hivyo nilichokifanya ni kutulia tu kitandani nikawa nasikilizia muziki kupita spika ndogo za masikioni “Earphone”.
Nililikuwa nasikiliza nyimbo laini za kizungu, nilijisikia burudani mpaka moyoni.
Nilisikiliza nyimbo baadae nilichoka nikatoka nikaingia youtube nikaanza kuangalia muvi.
Kuna muvi moja ilinivutia sana kuna mwanamke fulani katika muvi ile alinivutia sana jinsi alivyokuwa akicheza muvi ile kwanza alicheza kwa kujiamini mno halafu mkono alikuwa anauweza hatari, kipigo alikuwa anagawa kama dozi.
Kingine umbile la mwanamke yule lilinivutia, kwanza alikuwa namba nane halafu mwili wake ulijaa vizuri huenda sababu ya mazoezi, muvi ile ilinipeleka mpaka majira ya saa nne na nusu ndipo simu ya Sam ilipoingia.
“Hallo…” Nilipokea.
“Nimefika Chek point mke wangu.”
“Sawa onana na mhudumu yeyote apo akulete chumba namba 3.”
“Sawa.”
Muda mfupi baadae mlango uligongwa nikajua Sam ameshafika.
Nilishuka kitandani nikaenda kufungua mlango.
“Waooo! Mume wangu nilikukumbukaje jamani…”
Nilimkumbatia nikambusu mabusu yasiyo na idadi kisha nilimwachia akaingia nikafunga mlango.

Sam alienda kitandani akaketi, nami nilifika nikamkalia mapajani, yaani kiufupi siku hiyo nilikuwa na hamu sana ya kufanya mapenzi na Sam.
Kuna wakati hata nilihisi mwasho fulani hivi wa kukera, nahisi hata Sam alilitambua hilo kwani kuona vituko vile akaniweka kwenye njia na mimi nikaingia kwenye mfumo, tuliingia kwenye michezo ya hatari sana michezo ambayo baadae ilinitoa ufahamu.
Mwisho nakuja kushituka mwili unakakamaa kisha maji mengi sana yalinitoka kwa kasi kama risasi sehemu zangu za siri yakamrukia Sam tumboni wakati huo yeye hata kunijua alikuwa bado, jamani kuna watu mafundi siyo siri.
Nilichoka!
Nikabaki nahema tu.
“Vipi?”
Aliniuliza huku akinitizama usoni.
“Mbona hivi halafu mapema sana ee?”
“Toka uko.”
Nilianza kujigeuza, uke ulikuwa umeloa ute mwingi sana hata nikaona aibu.
“Tulia basi mbona unaanza kunikimbia tena?!”
Akanishika miguu akanipanua kitanda kikashuhudia jambo la siri.
Hakika katika siku ambazo nilifurahi tendo la ndoa katika maisha yangu yote basi siku hii ilikuwa ni mojawapo, hatua ya mwisho Sam anashuka kifuani kwangu aliniacha na majasho kila mahali kuanzia kwenye matiti, shingoni, tumboni hata mapajani.
“Asante Sam, nilikikumbuka sana hiki kitu tena saana.”
Nilimwongelea na sauti ya puani.
“Usijali kipenzi changu nilijua hili pia ni wajibu wangu kuhakikisha mke wangu unafurahi kila nikupapo haki yako.”
“Asante sana… Nafurahi sana maneno yako Sam.”
Akanibusu, nikajisikia furaha kuu moyoni.
Ama kwa hakika mapenzi ni matamu sana hasa yakikaa mahala pake, utafurahi mwenyewe.

Baadae tulitoka tukaingia bafuni tukaoga kwa pamoja kisha tulirudi chumbani tukajipaka mafuta kisha nilipiga manukato ya ukungu chumba kizima kuondoa shombo la ngono ili tupate kulala usingizi mnono!
Hata hivyo Sam alinishangaza na kitu kimoja ambacho sikukitegemea alipoaga kuwa yeye asingelala chek pointi kwa sababu usiku ule walikuwa na doria ya usiku ndani ya mji wa Iringa.
“Haa! Sam!”
Nilitahamaki.
“Kweli mke wangu.. Samahani kwa hilo.”
“Sawa.”
Niliitikia kishingo upande mno! Sikupendezewa.
“Usijali… Pia nafikiri hata kesho asubuhi sidhani kama tutaonana hata kukusindikiza nitashindwa!”
“Khaa!”
“Kweli… Lakini safari njema, nafikiri tutaonana hata uko ninaweza kuja wakati wowote kwaajili yako mpenzi.”
“Kweli Sam?”
“Ndiyo!”
Alijibu huku akinitizama usoni, nikamsogelea tukakumbatiana tukapeana mabusu kisha tukaagana kirefu zaidi.
Baadae Sam aliondoka akaniacha chumbani, moyo uliuma siyo siri.
Nilifunga mlango kwa ndani kisha nilijitupa kitandani, nao usingizi unanichukua mapema nafikiri ni kwa sababu ya shughuli niliyokuwa nayo muda mfupi uliopita.

Nilikuja kushituliwa na sauti za majogoo waliokuwa wakiwika kwa sauti majumbani mwa watu kuashiria kumekucha!
Nilikurupuka kama mwehu nikachukua simu yangu na kuiwasha kioo nikaona saa kumi na moja na dakika kumi na tano! Hee!
Nilichanganyikiwa baada ya kukumbuka saa kumi na mbili kamili basi nililokata tiketi linaondoka kule stendi.
Muda wa kuripoti ofisi za basi hilo Iringa mjini niliambiwa ni saa kumi na moja na nusu alfajiri ili tupelekwe stendi kuu ya mabasi iliyopo Igumbilo iliyopo mashariki ya mji mbali kidogo!
Ooh!
Nilikurupuka kama mwehu nikaingia bafuni nikajimwagia maji haraka nikarudi chumbani nikabadilika haraka sana ndani ya dakika saba nilikuwa tayari.
Nilichukua mkoba wangu na vitu vyangu vyote nikatoka mpaka nje uzuri bar hii ipo karibu kabisa na barabara ya mtaa ule na kwa bahati nzuri kabisa natoka nikakutana na bodaboda anakatiza mitaa hiyo haraka nikamwita.
“Vipi dada?”
“Safi za asubuhi?”
“Njema karibu!”
“Nikimbize haraka sana ofisi za mabasi ya Majinja Express haraka naelekea kuchelewa!”
“Oooh! Kalia chuma dada halafu nipe dakika tatu tu!”
Nikapanda!
Pale pale boxer ikapigwa moto wa kutosha!
Jamani yule boda alinifurahisha jinsi alivyokuwa akikimbiza bodaboda yake tena kwa mbwembwe nyingi na udhibiti mkubwa wa pikipiki!
Ni kweli ndani ya dakika mbili na sekunde kama hamsini hivi tuliwasili ofisi za mabasi ya Majinja Express, nilimlipa bodaboda ujira wake nae akaondoka zake taratibu niliwasiri na kulipoti ndani ya ofisi husika saa hiyo zikiwa zimesalia dakika chache sana.
“Dada kuna daladala hapo nje tayari imekwisha wasili tafadhali chukua mizigo yako panda daladala hiyo.”
Aliongea mfanyakazi mmoja wa ofisi hizo.
“Sawa.”
Nilijibu kisha nilichukua mizigo yangu likiwemo begi langu kubwa la nguo kisha nikatoka, huko nikakuta tayari daladala imekwisha egeshwa huku taa zikiwa zinawaka.

Niliingia ndani ya daladala hiyo, dakika mbili baadae iliondoka ambapo saa kumi na mbili kamili asubuhi tuliwasili stendi ya mabasi ya mkoa wa Iringa ‘Igumbilo Bus Terminal’.
Basi la kampuni husika tayari lilikuwa limeshaegeshwa kwenye foleni abiria wote tulioletwa na daladala tuliingia kwenye basi huku kila mmoja akiwa na tiketi mkononi.
Nilifika siti namba 37 ndiyo siti niliyotakiwa kuketi kwani iliandikwa kwenye tiketi, begi langu kubwa lilikaa kwenye buti huku begi dogo nikiliweka kwenye buti la ndani, mkoba nikaupakata mapajani.
Dakika kumi baadae basi liliondoka, hakika ilikuwa ni safari iliyonifurahisha sana, nilifurahi sana moyoni kuona naenda kuliona jiji la Dar mara ya kwanza jiji linalosifika kwa kila aina ya sifa, nzuri kwa mbaya!.
Nikiwa safarini niliwasha data nikawa naperuzi mtandao, nilisoma taarifa mbalimbali za habari, nilipitia pitia pia baadhi ya tovuti baadae nilichoka nikazima mtandao nikaweka simu kwenye mkoba kisha nilisinzia nikalala usingizi mzito.
Ilikuwa ni saa saba na nusu tulikuwa Morogoro.

Saa kumi na mbili na nusu ilitukuta stendi ya Magufuli, nilizinduka usingizini nikashuhudia basi letu likiingia kwa kasi ya aina yake ndani ya stendi ile kubwa na iliyojengwa kwa ustadi wa hali ya juu.
Basi lilifika moja kwa moja eneo la egesho, likaegeshwa.
Abiria wote tulishuka, kila nilichokiona baada ya kushuka kilikuwa ni kigeni machoni pangu hata nikajisikia kero.
“Oya dada wapi?,. Mambo vipi lakini?”
Wapiga debe walianza kunisumbua hadi kero!
Nilichukia nikawakaripia hadi nao wakakasirika wakanitukana matusi ya nguoni nikawaangalia kwa dharau.
Mizigo yote ilitolewa kwenye mabuti, nikachukua begi langu nikaliburuza mpaka kwenye banda la kupumzika abiria hapo niliketi kiti mahali pa peke yangu nikatulia.
Baadae alipita muuza vinywaji, nikanunua soda na keki nikawa naburudisha mdomo pia wakati naendelea kupumzika.
Baadae nilimtafuta Erick hewani.
“Leylah.”
“Nambie.”
“Mambo?”
“Poa kwema?”
“Nimefika nipo stendi ya mabasi hapa.”
“Anhaa!… Sawa kwahiyo nije kukupokea?”
“Ndiyo fanya hivyo, sasa unafikiri mimi nitafanyaje wakati ni mgeni?”
“Sawa basi nakuja sasa hivi!”
“Sawa.”
Nilikata simu, lakini muda huohuo niliondoka, niliburuta begi langu kubwa la nguo mpaka nikatoka nje ya stendi hiyo nikatembea mita kadhaa nikakutana na bodaboda nikamsimamisha.

Nayo ikawa imetimia saa moja na dakika kumi, tayari kiza chepesi kilishaanza kutanda.
“Habari ya sasa hivi?”
“Poa dada karibu?”
“Samahani eti ni bar gani ambayo ipo karibu na eneo hili ambayo siyo maarufu?”
“Hapaa… Ni nyingi tu kuna nyingine ipo karibu hapo inaitwa Star Bar.”
“Naomba nipeleke hapo, shilingi ngapi?”
“Buku tu!”
“Sawa twende.”
Nilipanda bodaboda, nayo ikatiwa moto ambapo ndani ya dakika tano tuliwasili Star Bar nikalipa ujira bodaboda ikaondoka nami nikazama bar.
Huko nikanyoosha kaunta nikaulizia mhudumu wa vyumba, haikuwa kazi kumpata nikazungumza nae nikampa sababu za kikazi akaniwekea nikalipa hela ya mwezi iliyo na punguzo shilingi laki mbili na sitini elfu, nikajaza daftari kisha akanikabidhi chumba nikaingia na vitu vyangu.
Kutokana na uchovu mwingi niliokuwa nao ilibidi kwanza nijifungie nipumzike japo dakika kadhaa tu.
Nilianza kupanga panga nguo zangu vyema hasa baadhi ya nguo za kuvaa kuanzia siku ya pili yake nikazipanga panga vyema, hata kabla sijamalizia simu yangu ikapata kupigwa.
Nilivyoisabahi juu ya kioo nikaona mpigaji ni Erick.
Nikapokea.

“Hallo…”
“Nimefika stendi dada yangu.”
“Ooh! Samahani mpendwa… Nimeondoka kuna mwenyeji nimempata kwahiyo tutaonana kesho samahani kwa usumbufu lakini.”
Erick alichoka kusikia hivyo… Pumzi aliyoishusha iliashiria.
“Nisamehe.”
“Sawa.”
Alikata simu.
Niliitupia kitandani, nikaendelea na mambo yangu, mara ilipigwa tena.
Kuangalia mpigaji ni Sam.
“Waoo! Mume wa mimi.”
“Dah!… Kufika Dar tu, hata kunipigia sasa hutaki, utani huo Ley.”
“Hahahaha! Yes! Ni kweli unafikiri kufika Dar ni jambo jepesi?”
“Au siyo?!”
“Ndiyo.”
“Vipi lakini.”
“Safi tu, nimefika salama japo nimelala usingizi mkubwa sana kuanzia Morogoro.”
“Pole na uchovu wa safari mke wangu.”
“Asante pole na kazi pia mume wangu.”
“Asante ila leo pia tuna doria ya usiku hapa mjini.”
“Kwani mbona doria zimekuwa nyingi sana safari hii ndani ya mji?”
“Kuna uhuni unatendeka, mfano leo mchana kuna tukio la mtu kuuliwa mchana kweupe kisha kila kilicho chake limechukuliwa na wahalifu hawajabainika sasa hili linapelekea jeshi la polisi kufokewa na serikali ndiyo maana tumezidisha doria usiku na mchana.”
“Lo! Poleni pia hongereni kwa kulipigania taifa letu.”
“Asante mke wangu.. Vipi lakini umefikia wapi?”
“Nimefikia Bar.”
“Unakunywa?”
“Hapana… ndo nimechukua chumba bar.”
“We nae… Kwanini hukwenda hotelini?”
“Hapana nina kusudi langu kuchukua maamuzi haya.”
“Sawa mke wangu kazi njema.”
“Na kwako pia.”
“Asante.”
Simu ilikatwa nikaitupia kitandani, nikamalizia kupanga panga vitu vyangu.

Nikaingia bafuni nikaoga kisha nilirejea chumbani huko nilijipaka mafuta nikabadili nguo kisha nilijipulizia marashi kidogo, simu yangu nikaichomeka kwenye chaji kisha kutoka na kufunga mlango.
Nikaenda zangu ukumbini kwaajili ya kupata moja moto na moja baridi ili kuupa ubongo burudani, maana nilikaukiwa sana.
Nilitafuta sehemu tulivu, nikaiona taratibu nikajongea na kuketi ilikuwa ni sehemu ya kona iliyojitenga sana nikatulia huko.
Muda mfupi mhudumu alifika kunisikiliza.
“Niletee Kilimanjaro tano za baridi na glasi.”
Niliagiza.
Muda mfupi baadae nilihudumiwa, nilianza na glasi moja ya mpigo nikahisi kuchangamka.
Hapo nilianza kutafakari jinsi nitakavyoweza kutekeleza jukumu la kwanza kabisa la mauaji nililoagizwa kulifanya nikiwa Dar es Salaam.
Licha ya kupewa jukumu hilo bado sikujua ni kwa namna gani ningeonana na mtu huyo?
Sikujua ni vipi ningeweza kutekeleza jukumu hilo?
Kila nilivyofikiria kwa kina suala hili kichwa kilipata joto.
Nikanyanyua glasi na kupiga funda tatu za Kili-baridi nikatikisa kichwa baada ya kumeza pombe kwani nywele zilisisimka sababu ya msisimko wa pombe mwilini.
Baadae nilimwita dada mmoja aliekatisha mbele yangu.
Alikuwa ni mhudumu, alifika mara moja.
“Alienihudumia hapa yupo wapi?”
Nilimuuliza.
“Yupo kule mbele.”
“Niitie.”
Muda mfupi baadae mhudumu alienihudumia alifika kunihudumia.
“Unanidai shilingi ngapi?”
Nilimuuliza, nilitaka kulipa bili niondoke japo nilikuwa sijamaliza bia zangu.
“Asante dada lakini umeshalipiwa.”
Nilishtuka!
“Alienilipia ni nani?”
Nilimuuliza.
“Ni yule mkaka pale mbele.”
Aliongea yule mhudumu huku akioneshea mahali alipokuwepo yule mkaka.
Mmh! Niliguna moyoni.. nikajiuliza ananilipiaje bili mimi? Je, ananijua?
“Hebu niitie aje.”
Yule mhudumu aliondoka akamwita nae akafika nilipoketi.

Alikuwa ni mkaka hivi wa lika lakini usoni alionekana kukomaa sababu ya ugumu wa maisha kwanza ilionekana ni mtu anaeishi maisha ya kibabe sana mjini muonekano wake tu ulionesha.
“Mambo.”
Nilimsalimia huku nikimtizama, pia nilitaka nimgundue kama amelewa au? Ningeweza kugundua hilo kupitia ongea yake.
“Safi mzima?”
Alijibu!
Kupitia sauti yake niliweza kugundua kijana huyo hakuwa mlevi wala mvuta bangi labda alikuwa mnywaji tu wa kawaida sababu sauti yake ilikuwa imenyooka vyema kabisa.
“Karibu kiti.”
Aliketi bila hata wasiwasi, nami sikutaka kumlazia damu.
“Unaitwa nani mwenzangu?”
“Naitwa Jr!”
Jina lake lilinifanya nitulie kidogo! Jr hili jina halikuwa geni masikioni mwangu.
“Naitwa Leylah.”
Nami nikajitambulisha.
“Nafurahi kukufahamu.. ni jina zuri sana.”
“Asante kwa kunilipia vinywaji nilivyokunywa lakini kwanini umefanya hivyo?”
Nilimuuliza huku nikimtizama usoni.
“Aah! Nimekulipia tu lakini nisamehe kama nilikosea.”
Kupitia jibu lile niliweza kuelewa alichokuwa anakitaka hata macho yake yalieleza wazi, pia nikamwonea huruma.
“Hivi hauna mchumba huko mitaani?”
“Sina.”
“Kwanini?”
“Basi tu sijisikii kumiliki mchumba mtaani kwa sababu ya kuumizwa sana, nimeumizwa sana hadi nimekata tamaa ya kumiliki mchumba ndiyo maana nimeamua ili kuondokana na misukosuko ya mapenzi na misongo ya mawazo ni bora tu nitembelee sehemu kama hizi basi inakuwa poa zaidi sababu inakuwa ni nipe, nikupe basi.”
Wakati Jr anaongea hayo nilikuwa nimimtizama kwa makini sana usoni maana ake nisije kuwa nachotwa bila kuelewa.
“Sasa umejuaje kuwa mimi nakufaa kwa leo? Je kama hivi umeshajilipua elfu kumi halafu ishindikane?”
“Hiyo haina shida dada yangu na pia sikuwa na maanani juu ya hilo nimejiskia tu nikulipie moyo ndiyo umenituma hivyo ndiyo maana nikatanguliza samahani kama umekereka.”
“Hujanikera lakini mimi ni mke wa mtu.”
“Sawa siyo mbaya dada angu.”
Alijibu akaweka dalili za kuondoka.
“We unatumiaga kinywaji gani?”
Nilimuuliza kwa lengo la kumkawiza.
“Mimi natumia energy.”
“Hakuna pombe yoyote unayotumia?”
“Pombe kali kwangu ni castle lite.”
“Tulia basi niagize tunywe tupige stori au vipi?”
“Ah! Sawa dada yangu lakini namuogopa mumeo akitukuta tumekaa wote ni hatari kwangu.”
“Usiogope amesafiri.”
“Sawa.”
Nilimwita mhudumu nikaagiza bando mbili yaani bia kumi laini za castle lite.
Zilifika tukaanza kunywa, tuliongea mengi sana wakati huo mimi nilikuwa nategea ili nisilewe sana maana tayari nilishakunywa bia tatu za Kilimanjaro.
Jr alizipeleka mbili za chapu nikaona kachangamka, nikagundua huyu pia siyo mnywaji bali anadandia gari kwa mbele.
Maongezi yalikuwa mengi sana mwisho nilimuuliza swali.
“Hivi Jr unamjua Damson Mbalangu?”
Akanitumbulia macho!
DAMSON MBARANGU?

Hiviii Leylah upoje lakini we unaona kabisa tayari niko vyangu… Apa niko tungi halafu wanaiuliza kuhusu huyo mchungaji?
Haya sasa nikujibu nini?!

Sehemu 21 Sehemu 23
0
0