Hello! Karibu HASCAVELA

Muonekano wa Giza:

Msaada

Dunia Ya Pili - 15

“Ndiyo bado ninakupenda!”
Nilijibu ingawa halikuwa jibu kutoka moyoni.
Sam akacheka kisha akasema.
“Usipende kuwa mwongo Leylah.”
Aliongea huku akitabasamu.
Nilitulia huku nikimtizama usoni, kiukweli nilishakuwa na uoga juu ya Sam nilianza kumfananisha na kiumbe fulani wa kutisha!
Imani juu yake ikatoweka kabisa.
“Rudi ndani nitakukuta ninaenda kituoni mara moja.”
Alisema.
“Sawa.”
Nilijibu kisha niliondoka nikarudi ndani wakati huo ikiwa imetimia saa nane na robo mchana.
Mezani nilipomwacha mwanamama Angelina nilipakuta pakiwa na vinywaji pekee yeye hakuwepo.
“Huyu mama nae kaenda wapi?”
Nilijiuliza moyoni, lakini sikupata jibu.
Nilichukua chupa moja ya dompo ambayo ilikuwa haijafunguliwa nikaifungua na kumiminia pombe kwenye glasi hadi ikajaa nikaanza kunywa pombe ile kwa pupa kutokana na msongo wa mawazo nilioanza kuwa nao kichwani mwangu.
Nilikunywa glasi hadi zikafika tatu bado Angelina hakutokea.
“Mmh! Huyu mama inamaana kaondoka?… Mbona hakuniaga?”
Nilijiuliza huku nikisimama kitini, wakati huo tayari pombe ilishaanza kunichukua.
Nilitembea hadi mlangoni kisha nikasimama mlangoni macho yangu nikayatupa sehemu ya maegesho.
Mmh! Nilijikuta naguna kimoyomoyo, gari ya Angelina haikuwepo!
“Huyu mama kaondoka wakati gani?”
Nilijiuliza huku nikijitahidi kuvuta kumbukumbu ili nibaini muda ambao mama huyo aliondoka nikajikuta napo nakosa majibu.
Kwani muda wote nilikuwepo pale na Sam sehemu ya maegesho hata wakati naingia ndani ya bar gari ya Angelina ilikuwepo sasa nikajiuliza ni wakati gani aliondoka?
Sikupata jibu, hata hivyo niliamua kupotezea nikahisi huenda alikuwepo msalani na alipita pindi nakunywa sikumuona.
Nilijipa imani hiyo, hivyo nikarudi zangu mezani nikaendelea kunywa pombe bila hata wasiwasi.

Muda ulivyozidi kwenda ndivyo hivyo pia nilivyozidi kulewa baadae nikajikuta nimenyanyuka kitini nikaanza kuruka majoka huku na kule bila kujielewa.
Niliruka majoka huku nikiendelea kunywa pombe, mwisho unywaji ukawa wa hovyo kabisa baadae nilizima kabisa pasipo kujielewa.
Sikujua tena kilichoendelea kuanzia wakati ule na hata usiku wake.
Nilikuja kushituka asubuhi!
Napo kufumbua macho nikajikuta juu ya kitanda kikubwa cha sita kwa sita, kikiwa na godoro lake kubwa lililojaa vyema.
Duh!
Kutupa macho pembeni nilikutana na friji kubwa la vinywaji likiwa humohumo chumbani, upande wa pili kulikuwapo na redio kubwa ya sabufa aina ya Seapiano, kulikuwepo na meza ya kioo pamoja na kiti chake cha kiofisi ofisi, juu ya meza kulikuwapo na Tv ndogo pamoja na laptop kiufupi kilikuwa ni chumba chenye hadhi yake, kwamba kama kilikuwa cha mpangaji basi si haba mpangaji aliekipangisha alikuwa na pesa za kutosha au mfanyakazi kabisa.
Na bila shaka mpangaji alikuwa ni mwanaume kwa mujibu wa mazingira ya chumba chenyewe.
Mule ndani wakati nazinduka kutoka ulevini nilijikuta niko peke yangu…
Sasa ule muda nakisabahi chumba kile mara mlango ulifunguliwa.

Sam akaingia wakati huo akionekana kutokea bafuni kwani alikuwa na taulo pekee alilojifunga kiunoni huku akiwa ameloa mwili mzima.
“Sam…”
Niliita kimawenge huku nisijue akiitika ningeongea nini?
“Ooh!… Mke wangu umeamka wewe?”
“Ndiyo.”
“Umeamka salama?”
“Ndiyo nimeamka salama sijui wewe.”
“Mimi nimeamka poa pia.”
Nikashusha pumzi, nikakaa kimya moyoni nikiwa naelewa lazima Sam atakuwa na jambo moyoni kuhusu mimi… Na kweli, hazikupita hata dakika mbili mada ikaibuka.
“Halafu ni ulewaji gani uliouanzisha Leylah?”
“Kwanini?”
Nilijifanya sielewi ingali nilishajua fika anachomaanisha.
“Unakumbuka ulivyolewa jana?”
“Hapana sikumbuki.”
“Acha ujinga wewe!… Kwanini unakana kitu ambacho tayari umekwishakikumbuka?”
Aliwaka.
Nilitulia kimya huku nikimsoma usoni kama anapendwa na hasira au vipi.
“Haya wamekubaka mtungo watu watano! Jana usiku unakumbuka?”
“Tokaaa!”
Nilijibu kwa kiwewe huku nikikurupuka spidi kwenye godoro kisha nikapekenyua sehemu zangu nyeti na kuanza kuzikagua, neno la kuwa nimebakwa mtungo lilinizuzua akili.
Licha ya kukagua kwa umakini mkubwa bado sikuona kama nilibakwa.
Muda huohuo Sam alikuja na kuketi kitandani karibu yangu.
“Leylah punguza kunywa pombe mke wangu watakuja kukufanya kitu kibaya sana, jana nimekuta umezidiwa na pombe hujitambui umelala tu bar wanaume wanakufunua funua tu kila wakati ndiyo nikakutoa nikaja na wewe hapa.”
Aliongea Sam.

“Kwahiyo hapa ni wapi?”
Nilimuuliza.
“Hapa ni chumba ninachishi mimi.”
“Chumba au nyumba?”
Nilimhoji.
Chumba! Mimi ni mpangaji tu.”
“Kwanini sasa?”
Nilimuuliza ningali na mshangao mkubwa.
“Nimeamua tu.”
“Sasa gari unailaza wapi?”
“Gari hata nikiipaki popote pale inalala vizuri siku inayofata ninakwenda kuichukua.”
“Haa!”
“Ndiyo… Sema nini? Si unajua mimi ni askari polisi? Sisi tunaishi kwenye nyumba za serikali ila sasa mimi nimeamua kuwa na geto langu huku kitaa.”
“Mmh! Tangu lini Sam akawa askari polisi?”
Nilijiuliza kimoyomoyo.
“Mimi ni askari polisi kitambo sana, kwani umesahau kesi yako ya mauaji dhidi ya mume wako nani alikunusurisha? Si mimi?”
Nilishangaa Sam anajibu wakati sikumuuluza zaidi ya kujiuliza mawazoni.
“Ahaa! Kweli bwana nimekumbuka.”
Nilijibu huku nikisimama kutoka kitandani kwa lengo la kwenda msalani.
“Sasa unaenda wapi mke wangu.”
Aliongea Sam muda huohuo akasimama na kunikumbatia.
“Bwana mi nioneshe chooni wapi?”
“Chooni utaenda ila siyo saizi yaani asubuhi hii unaanza kuleta ratiba zako ningali na hamu?”
“Sam nitajikojolea bwana nimejibana muda mrefu ujue.”
Niliongea huku nikitaka kujichomoa mikononi mwake.
Mara nikahisi kidole kikiingia ukeni kwangu ni jambo lililonifanya nikapatwa na msisimko wa ajabu hata nywele zikaupokea msisimko ule mara mbili yake!
Oh! Kwani hata habari za chooni nilizikumbuka tena?
Wala hata sikuzikumbuka tena!
Wote kwa pamoja tukaingia kwenye mahaba, mahaba mazito yaliyojaa kila aina ya vionjo na utamu, mahaba yaliyodumu takribani robo saa nikajikuta niko hoi bin taaban huku uke wangu ukitoa utelezi mfululizo.

“Sam… Sam… Sam tafadhali aaah!”
Nilianza kujigeuza geuza tu kitandani tayari nilishakuwa na hali mbaya sana! Mwili, nafsi hisia na mawazo vyote kwa pamoja vilihitaji tendo la ndoa.
Kweli Sam alinielewa, alinigeuza nikakaa vyema basi tuliingia safarini.
Safari ambayo haikuchukua muda mrefu Sam alishuka huku akiniacha na jasho jingi kuanzia sehemu husika, kiunoni, tumboni, kifuani hata usoni.
Duh! Hakika kuna wayawezae haya mambo siyo siri kwani Sam aliniacha nikiwa mwepesi kama karatasi, hisia zilitosheka mno hata akili ikanikaa sawa.
Sam alinipa taulo nijipukute kisha akanioneshea mahali bafu lilipo.
Huko niliingia nikajimwagia kisha nikarudi chumbani ambapo nilimkuta Sam keshabadilika huku akiwa kavalia gwanda za kipolisi.
“Hivi kweli huyu ni polisi?”
Nilijiuliza ningali nimeganda nikimtizama kwanza Sam jinsi alivyopendeza ndani ya gwanda la jeshi la polisi.
“Hivi we Leylah.”
Aliniita Sam wakati huo akiwa kashika kichupa cha manukato akijipulizia.
“Abee!”
“We utakaa huamini vitendo zaidi ya maneno mpaka lini?”
“Kwanini?”
“Mbona ulikuwa huamini kuwa mimi ni askari polisi hadi ukaja kuamini hapa baada ya kuona nimevaa sare?”
Nilishituka!
“Siyo kweli bwana… Mbona nimeamini tangu muda ule umenipa maelekezo?”
“Ahaa!… Nikajua hukuamini.”
Akapotezea japo pointi yake ilikuwa ni ileile.
“Walaa…”
Kimya kifupi kikapita…

“Lakini Sam?”
Nilimwita.
“Nambie.”
“Ujue jana sikuelewa elewa pale Tembo bar?”
“Hukuelewa nini mke wangu?”
“Baada ya mimi kuvaa ile miwani niliona vitu vya kutisha mno! Halafu na wewe ukanitisha tisha pale kisha ukaondoka zako ujue nikikutizama sasa hivi sitaki kuamini kuwa nilikuona vile.”
“Ahahaha… Ile ni miwani tu ni aina fulani ya miwani ambayo imetoka huko Marekani ni miwani inayotumika kuchezeshea filamu za kutisha unajua nini?”
“Enhee!”
Nilikaa vyema kumsikiliza.
“Ile ni miwani ya wacheza filamu za kutisha!”
“Haaa!”
Nilitahamaki.
“Ee! Mcheza muvi anabandika camera ndogo kwenye ukope kisha akivaa ile miwani inayogeusa taswira ndipo hapo anaanza kucheza muvi ndiyo maana muvi zao za kutisha zinatisha kweli sababu wenzetu tayari wameshakuwa na teknoloji kubwa katika tasnia nzima ya filamu za kutisha.”
Ooh! Kufuatia maelezo ya Sam palepale nikakumbuka simu kutoka kwa Erick Dar es salaam.
“Halafu umenikumbusha kitu Sam, mwenzio nina dili la kwenda kucheza filamu Dar ujue.”
“Hahahaha! Hebu badilika kwanza tuondoke maana naenda kazini mwenzio.”
“Sawa.”

Hapohapo nilibadilika harakaharaka, kisha tukatoka.
Baada ya kutoka nje sasa, yale mazingira licha ya kuwa mgeni na sehemu yenyewe lakini mwonekano wa jiografia ile akili ilikataa kabisa kuamini kuwa ile ilikuwa ni Iringa.
Basi tukatoka katika nyumba ile licha ya kuwapo milango mingi lakini sikuona mpangaji hata mmoja.
Milango yote ilikuwa imefungwa, wala hakukuwa na dalili zozote za kuonesha uwepo wa watu katika nyumba ile.
Basi tukaondoka huku tukiendelea kuongelea mada ya mimi kwenda kucheza filamu Dar es salaam.
“Lakini ujue Leylah wewe ni mrembo sana? Muvi mtakayocheza watu wataipenda kwa sababu ya wewe!”
“Ahahaha! Acha utani bwana!”
“Kweli si upo utaniambia!”
Tulikata mitaa miwili tu! Mtaa wa tatu nikajikuta tupo soko kuu la Iringa tukitizamana na kituo kikuu cha polisi cha mkoa wa Iringa.
Uelekeo tuliokuwa nao ni kama tulikuwa tunatokea mitaa ya gerezani kule.
Nikashindwa kuelewa ile mitaa yote sikuwa naifahamu hadi nakuja kugutuka tupo hapa.
“Leylah ee! Baadae basi ngoja mi niingie kazini.”
Niligutushwa na sauti ya Sam pindi ananiaga.
Nikabaki nimesimama nikimtizama mpaka anafika getini, geti lilifunguliwa Sam akaingia huku askari waliokuwa getini wakimpigia saruti.

Sehemu 14 Sehemu 16
0
0