Hello! Karibu HASCAVELA

Muonekano wa Giza:

Msaada

Dunia Ya Pili - 27

“Tunashukuru sana kwa kujali uwepo wetu katika maisha na shida zako...
Tumepokea ombi lako la kuomba msaada juu ya kazi iliyopo mbele yako,
Damson Mbarangu ni kiongozi wa kidini mwenye nguvu kubwa mno!
Hawezwi kirahisi rahisi lakini sisi tunakuhakikishia kuwa Damson Mbarangu ataondoka duniani kivyovyote vile...
Lakini kwa shart moja tu! Kabla ya kuifanya kazi itabidi usafiri mpaka Makambako huko utafikia ‘Nyumbani tu!’
Utapikwa baada ya hapo utakuja kumwangamiza kirahisi sana! Lakini kabla ya hilo hudhuria sana kanisani kwake husika kwa kiasi kikubwa kwenye sadaka, misaada na michango hapo kanisani atauona uwepo wako kupitia kujitoa kwako kisha ataweka ukaribu na wewe utashirikishwa kwenye vikao mbalimbali vya kanisa na kadhalika atazidisha ukaribu sana na hiyo kwako itakuwa fursa kubwa sana kwako kukamilisha kazi kirahisi mno… Umenielewa?”

“Ndiyo.”
Nilijibu haraka.
“Kwaheri pia nikutakie usiku mwema!”
Ilipokwisha kuaga sauti hiyo, radi kubwa iliunguruma nalo giza likatawanyika kwa wakati mmoja, papo hapo mwanga wa taa ukarejea chumbani.
Nilibaki nimeduwaa nisielewe chochote, nilivyokumbuka tukio lililotokea muda mfupi uliopita nywele zilisisimuka hadi mwili ukadata!
Maajabu!
Niliinuka kitandani nilipokuwa nimejilaza nikavaa nguo safi, nikachukua mkoba wangu ndani kukiwa na bastola pamoja na simu, nikatoka nikaenda ukumbini huko niliagiza chupa moja ya mvinyo mwekundu nikatafuta meza ya peke yangu nikaketi.
Muda mfupi kidogo nililetewa kinywaji changu nikafunguliwa nikamiminiwa kwenye glass nikakaribishwa.
“Samahani niagizie nyama choma huko jikoni halafu waambie waniletee na kaugali kidogo.”
“Sawa.”
Mhudumu aliondoka nami nikaendelea kunywa taratibu huku nikisubili nyama choma.
Papo hapo nilimkubuka Jr.
“Huyu kiumbe yupo wapi?”
Nilijiuliza saa hiyo nikichukua simu.
Nikampigia.
“Hallo!”
“Poa mzima?”
Kupitia sauti yake niligundua tayari keshachangamka.
“Mimi mzima!… Uko wapi wewe?”
“Natoka geto naelekea StarBar.”
“Ohooo! Sawa bwana.”
“Wewe uko wapi.. Au unalala Magomeni?”
“Walaa!.. Mi nipo Star.”
“Ok sawa tutasomana mida kidogo basi au?”
“Sawa.”
Simu ilivyokata nikamtafuta Sam hewani.
“Leylah!”
Sam alipokea simu kwa kunitaja jina.
“Mume wangu!”
“Niambie.”
“Umeshindaje?”
“Salama habari ya kazi?”
“Njema habari ya kazi mwenyewe?”
“Mmh! Ni njema lakini kazi hii inaonekana kuwa ni ngumu kidogo sababu pia kufuli nyingi sana.”
“Pole…Lakini nina imani hautoshindwa nakuamini.”
“Sawa wacha nijitume.. vipi lakini leo upo doria?”
“Hapana sipo doria usiku wa leo.”
“Uko wapi sasa hivi?”
“Nipo Miami.”
Sam kusema yupo Miami karoho ka wivu kakaniingia nikajikuta natamani nimuulize ‘Upo na nani?’ ila nikaghairi.
“Punguza wivu mke wangu… Niko peke yangu.”
Alinijibu ingali mimi sikumuuliza kwa sauti ya kufikiria tu akilini.
Nilibaki nimeduwaa.
“Hivi mume wangu samahani nikuulize swali?”
“Niulize tu!... Hata hivyo ngoja tu nikujibu.… Iko hivi mimi siyo binadamu kama wewe bali ni mimi ni kiumbe tu nilie na mwili wa kibinadamu lakini akili na uelewa wangu ni mara hamsini ya akili na uelewa wako ndiyo maana ninao uwezo wa kutambua mawazo na hisia za mtu.”
Dah! Nikabaki nashangaa mithili ya mtu aliefumaniwa ugoni.
“Usiku mwema mke wangu nakutakia kazi njema.”
Simu ilikatwa huku ikiniacha kwenye mshangao wa nguvu.
Maneno ya Sam kwa mara ya pili yalipita kichwani kwa kasi mithili ya umeme.
“Niulize tu!... Hata hivyo ngoja tu nikujibu.… Iko hivi mimi siyo binadamu kama wewe bali ni mimi ni kiumbe tu nilie na mwili wa kibinadamu lakini akili na uelewa wangu ni mara hamsini ya akili na uelewa wako ndiyo maana ninao uwezo wa kutambua mawazo na hisia za mtu.”
Bado maneno hayo yaliendelea kujirudia rudia kichwani kama mkanda wa video.

“Dada vitu vyako ulivyoagiza hivi hapa.”
Nilishtuliwa na sauti hiyo ya mhudumu nikagutuka na kutoka kwenye kilindi cha mawazo.
“Ahaa! Asante nitapata na maji kidogo ya kunawa?”
“Ndiyo ninayo hapa.”
Alininawisha kisha akanitengea nyama na ugali nilioagiza nikaanza kula.
Nikamkumbuka tena Jr...
“Kwani huyu mbona hafiki?…”
Nilijiuliza huku nikichukua simu nikitaka kumpigia.
Kabla sijatoa hata pattern nikamwona akiingia tena kwa mwendo uliochangamka.
Kwa mbali nikahisi moyo ukifurahi na kupata ahueni.
“Mmh huyu nae anataka kuniteka na kitu gani mbona kuna wehu nauhisi juu yake?”
Nilijiuliza angali bado namtizama jinsi atembeavyo kunikaribia nilipo.
Alifika na tabasamu jingi!
“Mambo!”
Alinisalimia huku akikunja ngumi kuomba tano!
“Safi tu nambie.”
Nami nikamsapoti kwa kumpa tano vile vile.
Akacheka akavuta kiti na kujumuika nami mezani.
“Nyama hizi hapa Jr nimenunua baada ya kusikia unakuja nimenunua ya wote.”
Akajumuika nami mezani tukaendelea kula huku tukiongea mawili matatu.
“Halafu mimi nahisi ulifatiliwa.”
Moyo ulipiga paa!
Hata kabla sijauliza nipewe maelezo vizuri tayari nilishaingiwa na wasiwasi neno kufuatiliwa siyo zuri.
“Kwanini?… Na kina nani?”
Niliuliza maswali mawili kwa wakati mmoja!
Jr aligeuka huku na kule kuona kama kuna mtu angeweza kusikia maongezi yetu, akajirizisha na mazingira kuwa hakuna mtu angeweza kusikia maongezi yetu.
Akaendelea...

“Muda tumeachana pale darajani si ulichukua boda boda?”
“Ndiyo!”
“Enhee!… Kabla haujaondoka mi kuna mahali nilichepukia kwenye kibanda cha fundi simu, nikiwa pale nilishuhudia wakati unaondoka kuna crown ilikufuatilia nyuma…
Nilishituka ikabidi nichukue pikipiki ya mwanangu mmoja pale nikachukua koti na helment nikavaa nikaiungia gari ile muda uleule.
Ile gari iliwafataa mpaka uliposhukia mpaka unakutana na yule jamaa hadi mnaondoka ile gari ilijaribu kuwafuatilia lakini kuna mahali finyu mlipita wao wakakwama wakarudi… Kama unakumbuka kuna mahali mlikuwa mmesimama mnaongea ongea kuna pikipiki iliwapita karibu vuuuu! Hadi vumbi! Unakumbuka?”

Palepale nikakumbuka pikipiki aina ya Boxer domo la mamba ilivyotupita tukiwa mahali kwa fujo hadi Erick akaachia tusi la nguoni sababu alimpita karibu utafikiri alitaka kumgonga.
“Anhaaa! Kumbe ulikuwa wewe?”
Nilimuuliza huku nikimtizama usoni.
“Yaaa!”
“Mmh! Kwanini umefanya yote hayo?”

Sehemu 26 Sehemu 28
0
0