Dunia Ya Pili - 08
Nilisimama nikatoa simu yangu kwenye mkoba, kuangalia nikakuta mpigaji ni Sam, nilishituka.
“Hallo!”
Nilipokea.
“Uko wapi Leylah.”
“Apa niko Mlandege.”
“Unataka uende kule kwenu? Usiende nenda kesho.”
Nilishituka kusikia hivyo, swali likapita kichwani,
“Amejuaje nataka kwenda nyumbani?”
“Leylah nilishakwambia sisi ni ulimwengu wenye nguvu mbona unakuwa siyo mwelewa kila siku unajiuliza maswali hayohayo vipi?”
“Aha! OK nimekuelewa.”
Nilijibu.
Sam akakata simu, nami nikashusha pumzi,
“fuuuh…”
Dah haya maisha nyie acheni tu.
Kwanza kichwa kilizima kwa muda nikakosa mwelekeo, nisijue nini nifanye wala niende wapi?
“Ah! Hapa bora niende zangu Miami tu.”
Nilijisemea moyoni, wazo la kwenda bar likapita kichwani nikalikubali kwa asilimia mia.
Papo hapo nilidandia bajaji iliyoniacha Miami bar, bila kupoteza muda niliingia ndani nikapanda ghorofani kabisa sehemu ya VIP.
Huko nikatafuta meza iliyojijenga nikaketi huko peke yangu, muda mfupi baadae mhudumu alifika kunisikiliza.
“Niletee Serengeti lite bando mbili na Malta makopo mawili.”
Mhudumu alileta kama nilivyomwagiza, Serengeti lite sita na makopo mawili ya Malta nikaanza kuburudika.
Wakati nakunywa nilikumbuka kuwa kwenye simu yangu kuna GB 50 za ofa hazijaisha bado haraka nilitoa kwenye mkoba nikawasha
data nikaanza na WhatsApp.
Huko nilikutana na vijembe vingi inbox bila kusahau vitisho vya kila aina kutoka kwa ndugu wa marehemu Meddy.
Sikuwajibu niliishia tu kuziangalia jumbe zao kisha nikazipuuzia.
Nikaingia status huko niliona status ya Amina haraka nikaifungua nikakuta kajipost akiwa kashika mshumaa huku akiwa kajifunika kikoi kichwani.
Kulikuwa na status mbili, ya kwanza ndiyo hiyo ilikuwa ya picha, nikaifata ya pili hiyo ilikuwa ni video fupi, ilionesha jinsi kaburi Meddy lilivyo
lakini ile video nilishindwa kuitizama kwa sababu ilirekodiwa wakati wa maombi sasa kila nilivyojaribu kuitizama nilihisi kitu mfano wa tonge la ugali
likija kwa kasi kutoka tumboni na kuja kunikaba kooni hali hiyo ilijirudia kila nilivyojaribu kuitizama video ile, mwishowe nilighairi na kuipotezea.
Nitizama status zingine mwisho nilitoka WhatsApp nikaingia Facebook, huko nilikutana na taarifa nyingi sana nilivyofungua nilikuta nyingi zinahusu
picha yangu, haraka nikafungua taarifa moja huku nikiwa na hamu kubwa kuona watu wameandika nini kuhusu picha yangu.
Kwanza nilishituka na kushangaa picha yangu ina like na maoni mengi utafikiri mtu fulani maarufu vile, kwanza nililainisha koo kisha nikakaa vizuri
nikaanza kusoma maoni yaliyotolewa kwenye picha yangu.
Maoni ya nice, beautiful, umependeza na kadhalika ndiyo yalikuwa mengi ila kuna maoni niliyovutiwa nayo yaliyosomeka hivi…
“Hey we mdada hiyo Apple umeitoa wapi? Mbona nembo yake sijaiona kwenye picha za wadada maarufu?”
Yale maoni yalinivutia, nikamwangalia huyo mtu kama yupo hewani ili nimjibu nikaona kweli yupo hewani, nikamjibu.
“Kwanini?”
Akajibu.
“Apple G36+? Ina GB ngapi kwanza?”
Nikamuuliza.
“Umejuaje kama ni Apple G36+?”
Akajibu.
“Nimeona nembo yake kwenye picha yako chini.”
Nilivyasoma yale maoni nikaingia kwanza kwenye system ya simu nisome maelezo yake ili nimjibu swali lake.
“Ram GB 32, storage GB 500.”
Nilimjibu kisha nilitoka kabisa mtandaoni nikaendelea kunywa pombe.
Wakati naelekea kulewa kuna mwanaume alikuja pale nilipokuwepo na kukaa karibu yangu nilivyomtizama nilimwona ni mbabembabe fulani hivi anayejiamini sana.
“Mambo?”
“Poa.”
Kama alivyosalimia nami ndivyo nilivyomjibu.
“Samahani ninaweza kupata kampani yako mrembo?”
“Hapana… Halafu kwani hukuona kiti kingine hadi uje kunibana hapa?”
Nilimuuliza kwa shari, yaani katika kipindi hiki nilijikuta nakuwa mtu wa kujiamini amini sana hata sijui hii hali ilitokea wapi.
“Kwani hutaki? Lakini hii ni sehemu ya bar huwezi kunipangia pa kukaa, hata hapa pia ninaweza kukaa kwani hata mimi pia ni mteja.”
“Sawa.”
Nilimjibu kifupi, tayari alishanipandisha hasira ndiyo maana sikutaka kuendelea kuongea nae.
Hata hapo nikaona hapanifai nilinyanyuka nikataka kuondoka.
Yule mwanaume akanishika mkono, nikageuka na kumtizama usoni.
“Tafadhari ninaomba kampani dada yangu hata kwa story tu nitaridhika samahani lakini.”
Nikaona kuendelea kubishana nae italeta picha siyo nzuri hivyo niliamua kukaa ili nione lengo lake nini haswa.
Niliketi akaagiza vinywaji vya kutosha hadi pombe kali aliagiza tukaendelea kunywa, aliongea mambo mengi aligusia hadi mahusiano
jinsi alivyosalitiwa siku chache zilizopita ndiyo maana amejikuta amekuwa mnywaji kupitiliza.
Aliniambia yeye ni mtumishi serikalini ni mtu mwenye pesa nyingi sana lakini mahusiano kwake imekuwa changamoto anaumizwa kila anapopenda.
Aliongea mengi huku tukinywa pombe hadi nikahisi naanza kuzidiwa na pombe lakini sikujali niliendelea kunywa sambamba na yeye pia!
Mwanzo sauti zilikuwa chini, lakini kadri muda ulivyozidi kwenda tukajikuta tumeanza kuongea sauti za juu sababu ya ulevi.
Muda uliyoyoma jioni iliingia hatimae usiku ukawadia baadae nilichoka kabisa, nilililewa sana nikaanza kuyumba tu kitini mfano wa mtu anaesinzia.
“Naona umezidiwa mrembo tumalizie basi glasi hizi nikusindikize ukapumzike.”
Aliongea mwanaume yule saa hiyo akijaza glasi hizo lakini pindi glasi zile zimejaa kuna tukio alilifanya.
Kuna bomba la sindano alilitoa kutoka mfukoni kwake bomba lile lilikuwa na kimiminika fulani akakiminyia kimiminika kile kwenye glasi moja kisha
glasi hiyo kwa umakini mkubwa huku akinichunga usoni aliisogeza upande wangu asijue kuwa niliona tukio lile.
Kumiminika hicho kilikuwa kibaya sana sababu kilikuwa hakibadilishi kitu chochote kwenye glasi kinywaji kilibaki vilevile.
“Kaweka nini huyu kwenye hii glasi?”
Nilijiuliza huku nikizidi kupatwa na ulevi wa kutosha.
Glasi yake alionja kidogo akaitua kisha akawa bize na simu.
Pale pale kwa utaratibu wa hali ya juu na usiri mkubwa mno nilimbadilishia glasi pasipo yeye kuelewa kisha nikanyayua iliyokuwa yake nikanywa
hadi ikashuka nikaitua upande wangu karibu kabisa na mimi huku nikiwa makini sana japo niliendelea kuyumba kilevi.
Haukupita muda mrefu yule mwanaume aliokota glasi akainywa ikashuka nusu ya katikati kisha akaitua, nikafurahi moyoni.
Hazikupita hata dakika tano alilala ghafla usingizi wa kutisha.
Haraka nilienda kuonana na mhudumu wa vyumba nikachukua chumba kimoja, nikaja kumkokota, mpaka chumbani huko nilimlaza kitandani haraka sana nikaanza kumsachi,
nilimkuta akiwa na pesa kiasi cha shilingi laki nane, kadi mbili za benki CRDB na NMB, bastola na kitambulisho chake cha kazi.
Nilichukua vyote kisha nilimwangalia mwanaume yule nilitamani nimuue kabisa lakini nikamwonea huruma nikamsamehe ingawa sikujua lengo la kutaka kuninywesha
dawa ile kali ya usingizi lilikuwa nini.
Baada ya kumsachi na kuchukua vitu vyake niliondoka zangu.
Nilitoka bila kutizamana na mtu hata mmoja.
Tayari ilishatimia saa tatu kasorobo usiku.
Baada ya kutoka niliita bodaboda, haraka mmoja alifika hapo.
“Nipeleke Serengeti bar.”
“Ni shilingi elfu mbili.”
“Twende.”
Nilipanda tukatoka.
Tulipita maduka ya sokoni hapo nilinunua maziwa Makopo mawili, nikanywa moja ili nipunguze pombe kichwani, tukaendelea na safari.
Serengeti bar hapakuwa mbali tulifika muda huohuo, nikamlipa dereva bodaboda ujira wake akaondoka zake nami nikaingia zangu bar.
Cha kwanza nilichokifanya ni kuchukua chumba kisha nikaufungia mkoba wangu uliokuwa na mzigo huko chumbani nami kwa mara nyingine tena nikaingia
ukumbini kuendelea kupata moja baridi moja moto.
Kwanza nilienda jikoni nikachagua nyama ya kitimoto steki ya mafuta nikaomba nichomewe ya shilingi elfu tatu.
“Fanya upesi kidogo.”
“Sawa bosi.”
Nilirudi ukumbini lakini safari hii sikujisikia tena kunywa pombe japo nilitamani sana kunywa pombe lakini sasa mtima ukawa hauzitaki,
hivyo niliagiza tu Serengeti lite mbili za kupotezea muda.
Nilinunua na Grand Malta moja ya kopo nikaendelea kunywa taratibu vinywaji vyangu hadi nyama zikaja nikala.
Baadae nilianza kuhisi usingizi nikaona bora nikalale tu.
Niliondoka nikaenda zangu chumbani.
Huko nilipunguza nguo nikapanda kitandani niliichukua simu yangu nikaangali saa nikaona ni saa nne na dakika kumi.
Nilichokifanya ni kuiweka simu yangu earplane mode ili kuepuka usumbufu wa simu za usiku, nikaweka pembeni kisha nikatoa bastola ile na kuiweka
kitandani pembeni, halafu nilijifunika shuka tayari kwa safari ya kuusaka usingizi.
Kabla hata sijalala mara nilisikia muungurumo wa gari aina ya land rover ikija na kusimama nje ya bar ile punde si punde nilisikia mtu katandikwa bonge la banzi.
“Paaaaaah!… Sema wapi?”
“Humu ndani?”
Moyo ukaruka tah! Sauti iliyojibu “Humu ndani.” Niliitambua fika.
Ndiyo maana nilikurupuka kitandani kama mwehu nikakaa huku moyo ukianza kwenda puta.
Muda huohuo nikasikia purukushani zimefika ukumbini, hadi kaunta nilisikia wahudumu wameanza kutembezewa kipigo huku wakitakiwa kuonesha ni chumba kipi
alicholala mdada aliyekuja na bodaboda muda mfupi uliopita, mbaya zaidi dereva bodaboda mwenyewe walikuwa nae hapo nilimsikia nae akihojiwa na kutoa
maelezo kuwa kweli huyo mteja alimfikisha hapa Serengeti bar.
Kipigo kilitembea hadi kwa wahudumu wote huku nikiwa nasikilizia, mwisho purukushani zikasikika zikija nilipo niliduwaa nikahisi haja ndogo inataka kuniponyoka.
“Oohps! Nini hiki tena?”
Nilijiuliza huku nikishuka kitandani nikasimama.
Mara walifika mlangoni.
“Ni hap…”
Kabla sentesi haijakamilika mlango ulifunguliwa kwa teke bastola zikatangulia huku watu waliovalia magwanda ya polisi wakifata nyuma.
Unaweza pia kusoma: