Hello! Karibu HASCAVELA

Muonekano wa Giza:

Msaada

Dunia Ya Pili - 26

Yaani sikupata jibu nikaishiwa kuduwaa tu!
“Yaani hata nilivyochukuliwa na usingizi unafikiri nilielewa basi?” Niliongea huku nikicheka kinafiki japo moyoni bado nilikuwa na maswali mengi Sana juu ya kile kilichotokea muda mfupi uliopita.
“Pole sana!”
“Asante.”
“Unajua nini Leylah… Muda nafikiri umekaribia kwahiyo ingelikuwa vyema zaidi tuanze kusogea mazingira au unasemaje?”
“Ni sawa.”
Ikiwa ni saa tisa kasoro arasili tukiwa mimi na mwenyeji wangu Jr tuliondoka K.Pub moja kwa moja safari ikawa ni kusogea mahala lilipo kanisa la mchungaji Damson Mbalangu.
Hapakuwa mbali kwani baada ya mwendo kama wa dakika saba hivi nilianza kusikia mdundo wa miziki ya injili.
“Unausikia huo muziki?”
Aliniuliza Jr.
“Ndiyo!”
“Basi ndiyo hapo!”
“Sawa.”
Nilijibu huku moyo ukuanza kuingiwa na ukatili mkubwa sana juu ya mwinjilishaji wa kanisa hilo mchungaji Damson Mbalangu.
“Lakini ukiachana na uinjilishaji, mchungaji huyu maisha yake ya mtaani yakoje ana huruma kwa watu kama ilivyozoeleka kwa wachungaji na watawa wengine?”
Nilimuliza swali la akili.
“Yaa! Anasaidia sana watu! Lakini ameua ndoa za watu wengi sababu misaada yake imepelekea baadhi ya wanawake kuwadharau waume zao.”
“Una maana gani kusema ameua ndoa za watu wengi?”
Nilimuliza saa hiyo umakini wote wa akili, masikio na macho vikiwa kwake.
“Ah! Si unajua wanawake na pesa ni sumaku na chuma?… Hivyo misaada ya mchungaji huyo kwenye familia zao imefanya apendwe yeye kuliko wanaume wenye familia.”
“Mmh! Sasa yeye si mchungaji?… Si anakuwa anatoa misaada tu?”
“Wakijipendekeza anaruka nao vizuri tu mbona nae damu inachemka?”
Nilicheka moyoni kusikia hivyo, nikajua huyo kweli siyo mchungaji bali ni kiumbe fulani hivi wa kutisha aliejivika sura ya uchungaji.

Tulifika eneo la kanisani ikiwa ni saa tisa na dakika tatu alasili tayari watu walishaanza kukusanyika, kanisa lilikuwa zuri kwa kulitizama lilijengwa kwa ramani ghali sana na ya kisasa zaidi.
Ndani ya kanisa hili kulikuwa na bustani kubwa sana iliyokuwa ikihudumiwa ipasavyo, kulikuwa na viti vizuri na vya kila aina kwaajili ya kupumzika kiufipi ile ilikuwa ni bustani ya starehe.
Tukiwa na Jr tulitembea tembea sehemu ile ya bustani tukasafisha macho, tuliongea mengi mwisho kengele ya kuanza ibada iligongwa.
Ndilo gari nzuri kama ya mbunge yaani land cruiser v8 nyeusi iliyovimba iliingia pale kanisani nikiwa mita kadhaa niliikazia macho ile gari hadi inaenda kuegeshwa sehemu yake ya maegesho.
Walitangulia kushuka wanaume wawili mbavu kiasi waliovalia suti nyeusi za kufanana, baadae ndipo akashuka kipande cha mwanaume wa miraba minne!
Akiwa ndani ya suti ya bluu shingoni akiwa kanyonga tai ndogo nyekudu yenye mwonekano wa kipepeo.
Alishuka pia mwanamama ambae bila shaka akili yangu iliambia huyo no mkewe mchungaji, hili lilidhilisha kwa sababu alikuwa amebebelea mabiblia mkononi mwake.
Waliingia kwa pamoja kanisani huku nasi baadhi ya waumini tuliokuwa tumesalia nje tulifata nyuma.
Ibada ilianza saa kumi kamili lakini ilipotimu saa kumi na nusu mi na Jr tuliondoka kwa kuwa kilichonipeleka pale nilishakitimiza hivyo sikuona haja ya kuendelea kuwepo pale, tuiondoka.

Tulirudi mpaka Manzese darajani hapo ilibidi niachane na Jr.
“Jr asante sana!… Nafikiri tutaendelea kuwasiliana na hata kuonana pia sawa?.. sasa hivi ninahitajika kufika Magomeni.”
“Ahaa! Usuwaze dada angu!”
Alinipa mkono.
“Tutaenedelea kuwasiliana pia.”
Alisema.
Tukaachana.
Nilitamfuta Erick hewani na nikampata alinielekeza ni wapi walipokuwa wakifanyia mazoezi kwa mara ya kwanza nilienda kuungana nao nikaanza mazoezi rasmini kwaajili ya kurekodi video ambayo niliombwa kushiriki.
Kila kitu kilienda sawa jioni ile, nilifanya mazoezi mawili kwa wakati mmoja nilifanya zoezi la kuendesha gari pia la kuigiza, kazi kwangu ilionekana kuwa nyepesi mno tofauti kabisa na nilivyotegemea, hata Erick mweyewe akanipongea Sana.
“Una kichwa chepesi sana Leylah unaweza kuja kuwa mwigizaji mzuri sana hapaa nchini hapo baadae ongeza bidii.”
“Asante Erick nashukuru na nitaongeza bidii.”
“Kwahiyo sasa hivi baada ya zoezi si tunaelekea mahali nilipokutafutia chumba?”
“Hapana!.. Asante kuna sehemu tayari nina chumba kwahiyo usiwaze.”
Niliongea kwa tabasamu japo yeye hakupenda nilimuona kabisa.
“Sawa.”
Alikubali kishingo upande sana!
Sikumtilia maaanani tuliagana na tukaachana kabisa!
Nilirudi mpaka nilipochukua chumba StarBar.
Cha kwanza ilibidi kwanza nioge ili kuweka mwili sawa, baada ya kuoga nilijilaza kitandani, kichwani nilianza kuchora ramani namna nitakavyoweza kummaliza Damson Mbarangu.
Haikuwa kazi rahisi sababu kwanza alikuwa na ulinzi wa mabodigadi hivyo ulihitajika umakini mkubwa sana kuhakikisha nafanikisha hilo zoezi, ilihitajika akili kubwa mno!
“Upo huru kumteka mwanaume yeyote yule kimapenzi ikiwa kwaajili ya maslahi, lakini angalizo! Usichanganye kazi na mapenzi.”
Maneno ya Sam yalipita kichwani mwangu kama mkanda mfupi wa rekodi ya sauti, nikashusha pumzi nzito.
“Fuuuuuh!”
Papo hapo nilikujiwa na kumbukumbu nyingine akilini...
“Ni hivi… lile kanisa linaendeshwa kwa nguvu kubwa ya kishirikina nguvu ambayo mchungaji huyo aliitoa huko Nigeria hivyo siyo wa mchezomchezo kama unavyomzania!..
Halafu kingine sasa usichokijua! Unaelekea kugonganisha nguvu tatu kwa wakati mmoja, ujue kifo chako kitakuwa kibaya sana!”

Akili ilizidi kupata moto siyo kwa mitukio hiyo! Hapo hapo nikakumbuka lingine!
“Mjukuu wangu Leylah.. umeingia katika agano gumu mno! Upande wa ukoo wako! Lakini pia kuna agano linakusubili upande wa mama yako! Mama yako aliniambia wewe ndiye mwanae mpendwa utakaemiliki mikoba yake, lakini kwa bahati mbaya alifariki pasipo kukumilikisha mikoba hiyo sababu ulikuwa bado mdogo.”
Doh!
“Na sasa wakati ni huu! Mizimu inahitaji umiliki wako kwao nami nakufanyia tambiko hapa chini ya mkuyu ukawe mtu mwenye nguvu, tajiri pia mwenye nguvu kimamlaka kwa watu wote waliochini yako!.. Nitakupatia hilizi, ni hilizi ambayo itakuwezesha kuwasiliana nasi muda wowote utakao, utaomba chochote utapewa lakini kwa sharti moja tu! Kila ifikapo tarehe saba mwezi wa saba itakubidi usafiri mpaka Lupembe kunako mkoa wao Njombe, kuna mkubwa wetu huko atakufanyia miungu midogo midogo na utazidi kuimarika kiuchumi hata kinguvu pia!”
Nilipokumbuka hayo maneno kuna akili ilinijia kichwani, kwanza nilichukua mkoba wangu nikasachi na kutia hirizi niliyorisishwa kimazingara usiku wa kuamkia siku hiyo.
Niliibinya binya kisha niliongea na mizimu kama jinsi nilivyoelekezwa na bibi.
Ghafla tu taa ikazima kiza kizito chenye kutisha kikatanda chumba kizima sauti nzito ya kibabu ukasikia ikinena kwa kusema...

Sehemu 25 Sehemu 27
0
0