Dunia Ya Pili - 13
“Vipi?”
Aliuliza mhudumu yule ilihali akiwa katika hali ya tahamaki.
“Ah!… Samahani niliota ndoto mbaya ndiyo sababu ya hili lililotokea.”
Nilijibu.
Akabinua midomo yake kwa dharau sababu ya adha ya usumbufu, akaondoka zake.
Nilinyanyuka kitandani nikaingia bafuni huko nilivua nguo nikajikagua vizuri kweli nilikuta nimeingiliwa kimapenzi kwani baadhi ya sehemu
zangu nyeti kama matiti na usichana wangu vilikuwa vimelegea sana ngozi kana kwamba nilitoka kujihusisha kingono muda siyo mrefu.
Papo hapo kumbukumbu zikanijia, nikapata kukumbuka ya kuwa muda mfupi nilikuwa na Sam kule kunako Dunia ya pili.
“Mmh! Yule mkaka ni mzuri na kazi anaiweza jamani mmh!”
Nikajikuta nafikiria upuuzi hata hisia zangu zikashituka.
Nikiwa bafuni nilioga vyema, na kwa kuwa nilitoka nyumbani huko nilitoka na baadhi ya nguo zangu hivyo nilivyorudi chumbani nilibadili nguo
nikavaa zingine kisha nilijipaka mafuta nikajipulizia na unyunyu.
Nilichukua mkoba wangu wenye pesa nikatoa kiasi cha laki tatu nikakiweka mfuko wa kushoto wa gauni kisha nilitoa bastola nikaiweka mfuko wa
kulia wa gauni, halafu ule mkoba niliutumbukiza kwenye begi lenye nguo zangu chache pamoja na jiwe kubwa la dhahabu nililotoka nalo nyumbani kwa wakwe.
Baada ya hapo nilichukua begi langu na kulitupia mgongoni, nikaichukua simu yangu kisha nikawa natoka ndani ya chumba kile huku nikimtafuta Sam hewani.
“Ee! Leylah.”
Alipokea wakati huo nami nikiwa koridoni naelekea ukumbini kisha nitoke nje.
“Mambo.”
“Poa mzima mrembo wangu mimi.”
“Toka uko! Halafu wewe… Sikutaki hata.”
“Kwanini sasa?”
“Sitaki tu!”
“Lakini mimi nakutaka.”
“Utajua wewe.”
“Hahaha! Vipi lakini umeamka salama?”
“Yeah! Nimeamka salama hofu kwako.”
“Mimi pia ulivyoamka wewe, ndivyo hivyo nilivyoamka mimi.”
“Sawa, kwahiyo mimi ndiyo natoka sasa guest.”
“Ahaa! OK, sasa tukutane wapi?”
“Nikuulize wewe.”
“Hapaaa njoo stendi ya zamani hapa.”
“Sawa.”
Nilikata simu wakati huo tayari nikiwa nimetoka nje kabisa ya guest ambayo pia ni bar maarufu ya Five star.
Hapo sikutaka kujitesa kutembea ya mguu nilichukua bodaboda iliyonikimbiza moja kwa moja mpaka Stendi ya zamani Iringa mjini,
huko nikatafuta sehemu tulivu nikampigia Sam.
“Uko wapi?”
“Stendi ya zamani uliponiahidi tukutane.”
“Njoo Tembo bar hapa chini.”
“Tembo bar hata sipafahamu.”
“Chukua bodaboda mwambie akulete tembo bar wao wanapafahamu.”
“Sawa.”
Muda huohuo nikachukua bodaboda iliyonikimbiza moja kwa moja hadi tembo bar.
Ama kwa hakika ile nayo ilikuwa ni bar nzuri mno!
Kwanza ilikuwa na eneo kubwa la maegesho ya magari huko nje, achilia ukumbi mkubwa wa vinywaji mule ndani, achilia hadhi ya vyumba vya kulala wageni humo ndani,
acha uzuri na unadhifu wa wafanyakazi mule ndani.
Pia ilikuwa ni bar iliyosheheni huduma zote humo, hakukuwa na haja kwa mteja kutoka kutafuta huduma nje ya bar.
Huduma zote muhimu kama vile huduma zote za kifedha kuanzia huduma za kibenki na huduma za mitandao ya simu vyote vilikwepo ndani kwa ndani.
Na kubwa zaidi bar ilikuwa na huduma ya Wi-Fi, hivyo wateja wote ndani walitumia intaneti ya bure.
Ndiyo maana hata ikapendwa sana kwani asubuhi ile nilikuta watu wamejazana kama nyuki hata nisijue Sam ni wapi nitamwona kaketi, ikanibidi nimpigie simu.
“Hallo.”
Alipokea.
“Nimefika sikuoni.”
“Nakuja nimekuona.”
Alisema.
Kweli baada ya simu kukata Sam alitokea huku akiwa kalewa chakali hata macho yake yalikuwa mekundu.
Akanichukua pale akanipeleka meza iliyokuwa imejitenga pembeni lakini kukawapo na wanamama wawili wenye miili iliyodhihirisha kuwa pesa wanayo kwani
nywele zao zilisukwa misuko ya hela nyingi pia mikono yao ilikuwa imevikwa saa za vito vya dhahabu pamoja na pete zao pia.
Nami nikajumuika nao pale, nikawapa salamu zao nao wakanikaribisha mezani ambapo kulikuwapo na chupa nyingi za dompo.
Nami nilijumuika nao kwa kuchukua glasi nikaminina dompo tukaanza kunywa pamoja.
Baada ya kitambo kifupi Sam aliwatambulisha wale wanawake jina langu pia akanitambulisha kuwa mie ni mchumba wake, yaani mke mtarajiwa.
Wale wanawake nyuso zao zikachilia matabasamu ya furaha, wakanipa mikono nami nikapeana nao.
Baadae Sam akawaambia wale wamama kuwa nilikuwa nahitaji kupewa msaada kufikia ndoto zangu.
Nilishangaa kusikia kuwa nahitaji msaada! Je ni msaada gani unaohitajika kwangu pasi na mimi kuujua?
Sam aliewaeleza kuwa hata hapo nilipo nipo na jiwe kubwa la dhahabu lenye thamani ya kiasi cha bilioni sita za kitanzania lakini sikuwa na usimamizi
maalumu wa kuhakikisha naliuza.
Akawaeleza kuwa aliniahidi kunisindikiza nchini Afrika kusini nikaliuze kwenye soko kubwa la madini barani Afrika lakini sasa isingewezekana sababu
alipatwa na dharura ya kusafiri kwenda Nigeria ambapo huko angekuwa na ziara ya siku tano kabla ya kuingia Washington DC chini Marekani ambapo huko
atahudhuria mkutano mkubwa na viongozi wa dunia, baada ya hapo angekwea pipa mpaka Roma nchini Italia halafu ndipo arudi nchini hiyo ingemkawiza kidogo
ndiyo maana aliwaomba wale wanamama wanisaidie.
Sam kutaja zile luti nilijikuta naingiwa na shaukuu kubwa sana ya kutaka kujua huko kote anaenda kufanyaje jamani?
Mwanamama mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Angelina alimuuliza Sam kuwa hilo jiwe ni la shilingi ngapi?.
Sam akamjibu.
“Utalithaminisha wewe mwenyewe ingawaje halipungui bilioni sita.”
Aliongea Sam.
Hata nilipogeuka kumtizama tukatizamana ana kwa ana na macho yake mekundu yaliyoiva sababu ya ulevi mwingi aliokuwa nao.
Yule mama alitangulia kusimama nami nikamfata nyuma tukaenda mpaka nje, huko tukanyoosha sehemu ya maegesho, huko akachomoa land cruiser moja nzuri nyeusi
tii iliyokuwa imeegeshwa pamoja na magari mengine.
Akaigeuza na kusimamisha karibu yangu, nao mlango wa upande wa kushoto ukajifungua wenyewe.
Nikaingia nao mlango ukajifunga, saa hiyo mama yule nae akaweka limoti kwenye dashboard kisha akakanyaga mafuta gari ikaondoka.
Ilikuwa ni gari nzuri mno! Yenye kunukia marashi yenye harufu tamu puani, raha moyoni.
Humo ndani kulikuwa na mziki nyororo wa kizungu unaimba taratibu nao ikayafanya masikio yangu yafurahi.
Angelina akaendesha gari akaizunguka mashine tatu tunapita upande wa magharibi kisha tukaikamata barabara ya kuelekea mlandege ipitayo chuo cha VETA
nayo tukapanda nayo mpaka tukakikaribia chuo chenyewe lakini hatukukifikia tukachepukia pahala lilipo banda la kuoshea samaki huko tukakutana na
barabara ya vumbi iliyokuwa imeingia mitaani huko tulitembelea maili kadhaa yule mama akasimamisha gari lake.
Kisha alipandisha vioo vyeusi vya tinted vikafanya yeyote apiae nje asiweze kutuona ndani.
Hapo nikadaiwa kuutoa huo mzigo, nami bila hiana nikautoa ule mzigo nae akaupokea na kuitizama.
“Yeah hii kweli ni bilioni sita!”
Alisema.
Kabla sijajibu Angelina akaniwahi.
“Hivi binti waitwa nani kwanza?”
“Mimi?”
Nilitahamaki.
“Ndiyo wewe!”
“Naitwa Leylah.”
“Jina zuri, je watambua misingi ya kile unachokitumikia nacho kikakupa utajiri kama hivi?”
Aliongea huku akinionesha lile jiwe.
“Hapana.”
Nilikana.
“Sawa sasa tega sikio nikueleze.”
Nikatulia tuli huku nafsi ikihaha kutaka kulijua hilo.
Yule mama aliniambia kuwa mimi tayari nimeshakuwa mwanachama mshirika ndani ya chama cha Freemason akaniambia huenda nilikuwa sijui ila
kuingizwa kwangu katika ulimwengu huo ni agano ambalo liliwekwa miaka mingi na aliekuwa babu mkubwa kabisa katika ukoo wetu, na akaniuliza,
je sikupata kuzisikia sifa za babu yangu?
Nikamwambia nilisikia.
Akaniambia kuwa babu yangu alikuwa ni moja kati ya wazee wa zamani kidogo waliowahi kupata ufahamu mapema hivyo ufahamu wao ulipelekea
wafanye vitu vingi vya kuogopeka mfano mauji ya watu kisha kuchukua damu zao kisha damu hizo waliziuza kwa pesa kubwa sana nayo ikawa ni
kafara kwa watu wa Lucifer.
Baada ya kufanya biashara hiyo kwa kipindi kirefu babu yetu huyo nae alishawishika kuungana na wale waliokuwa wanunuzi wa damu,
akaungana nao, akawa mshirika mkubwa kwa Lucifer ndipo mwishoni mwa maisha yake shetani akamwekea jaribu baya kabisa katika maisha yake,
jaribu ambalo mwisho akapewa mtihani ili aepukane na adha ile ilikuwa ni lazima akaweke makubaliona na atie sahihi ya damu kwenye kitabu
cha kiapo mbele ya Lucifer kuiweka familia yake rehani pamoja na kizazi chake rehani ili yeye akombolewe na adha ile iliyomkumba.
Kutokana na uwoga juu ya uhai wake babu huyo akaiweka koo yake rehani tena kwa kutia sahihi ya damu kwenye vitabu vya Lucifer, ndiyo maana
kuanzia hapo ukoo ulianza kupukutika mwisho walibaki wachache lakini bado waliendelea kuisha hata kwenye familia ya bibi wakabaki wawili
baba marehemu na shangazi Jemima.
Marehemu baba alifanikiwa kuoa lakini nae baada ya kuzaliwa mimi walifariki na mama kisha nikabaki mkiwa ndipo shangazi akanichukua nikakulie kwake.
Hata hivyo nilikuwa ni mwenye kufariki lakini ikasemekana Lucifer kiongozi wa Freemason alipita msahama juu ya roho yangu ila akanitaka nijiunge
kwao ili nami nitoe kafara watu wengine.
Ndipo kwa mara ya kwanza wakamchukua mwanangu wa kwanza pindi tu nimetoka kujifungua, lakini baadae wakamchukua mume wangu Meddy kupitia mkono
wangu pasipo mimi kuelewa.
Lakini baadae wakaja kumchukua kijana mmoja aliyejaribu kunivamia akiwa na wenzake, wakamchukua pia kupitia mkono wangu lakini licha ya yote hayo
watu hao walipanga kunitajirisha sana ndiyo maana pesa ndogo kabisa kunipa walianza na bilioni sita ambayo mama huyo alisema anakwenda kuitoa lakini
kuanzia siku hiyo nitambue kabisa mimi ni nani, nipo wapi na nina nafasi gani?
Alihitimisha!
Nami nikameza matee huku nikijipukuta uso kana kwamba nilikuwa sioni vizuri.
Unaweza pia kusoma: