Hello! Karibu HASCAVELA

Muonekano wa Giza:

Msaada

Dunia Ya Pili - 29

Kwa sababu ya huruma nyingi iliyochanganyika na machozi vilivyoonekana kwenye paji langu la uso mara moja viliweza kuivunja vunja hasira ya Jr, pamoja na kuuporomosha msimamo wake wa kutaka kuondoka muda ule.
Alirudi akaketi kitandani huku akiwa bado analia kama mtoto mdogo, siyo siri kinauma hasa ukikoswa!
Nilimsogelea nikaketi karibu yake nikampukuta machozi kwa kiganja changu kisha nikajipukuta nami.
“Nisamehe.”
Niliongea kwa sauti ya chini sana.
Hakujibu aliishia tu kunitizama kwa macho ya bashasha,bado hakuwa na imani na mimi.
“Ninajua siyo rahisi Jr lakini ninaomba sana ujitahidi ujiweke sawa, uruhusu moyo wako uupokee msamaha wangu kwako ili nami nasfi yangu ikasuuzika… Najuta kwa kilichotokea nimeenda pupa mno! Najutia sikupaswa kufanya haya.”
Niliongea kwa hisia mno sauti yangu ilidhihilisha hilo.
Jr alitulia kidogo kisha akanigeukia na kunikumbatia kwa hisia kwa mikono yake miwili.
“Nimekupokea Leylah… Nimekusamehe japo haikuwa rahisi lakini imebidi tu nikisamehe sababu siyo mara yangu ya kwanza kukumbana na mikasa kama hii… kuna baadhi ya mikasa nimekumbana nayo katika maisha yangu huu ni mfano na siyo mkasa! Kuna mikasa ya kutisha nimepitia na nilisamehe sasa leo hii niwe nani nisikusamehe ewe ulieshuka chini ya miguu yangu ukiomba msamaha kwa machozi?…
Nitakuwa siyo muungwana nisipokusikiliza, kiufupi nimekusamehe Leylah.”

Nilihisi mwili mzima vinyweleo vimesimama, hakika huyu mtu alijua kucheza na hisia za watu, nasema haya kwa sababu maneno yake yalienda moja kwa moja kuigusa na kuitikisa ngome yangu ya hisia mahali ilipojengwa, nilishusha pumzi kubwa kupunguza presha niliyokuwa nayo moyoni muda wote ule tangu nazinduka usingizini.

“Asante kwa kunisamehe, ninashukuru mno bado nitaendelea kujutia leo na hata kipindi chote nitakachokuwa nawe.”
“Usijali Leylah wala hupaswi kufikiria kuhusu hilo sasa ganga na yajayo.”
“Asante.”
“Basi mi nafikiri nikuachie sababu kumekucha natakiwa niingia mtaani kufanya harakati, nafikiri tutaendelea kuwasiliana.”
“Sawa.”
Nilimwachia aende kwa sababu nilikuwa bado nimemkumbatia, mara kuna nafsi mbili zilianza kubishana moyoni, moja ilisema acha aende nyingine ikasema mzuie.
Ulikuwa ni mbishano mkali sana nikabaki nimeduwaa hadi anavyoshika kitasa cha mlango akaufungua.
Nilizidi kukumbwa na hali ya kuchanganyikiwa, nafsi zilizidi kubishana kwa nguvu nikajikuta nakosa amani.
Akapiga hatua ya kwanza kutoka chumbani, mara akapiga ya pili huyooo akawa anapotelea.
“Jr!”
Niliita bila kutarajia!
Aligeuka akanichungulia akiwa nyuma ya mlango.
“Nambie.”
“Kuna kitu nimesahau njoo kwanza tuongee.”
Nikamsogelea na kumwongelea sikioni…
“Halafu Jr mbona umenibaka wewe?”
Alidata akataka kuinuka nikamwahi nikamshika mkono akatulia!
“Mbona mi sijafanya hicho kitendo jamani kumbe ndiyo maana unataka kunipiga risasi?”
Aliongea kwa kutetemeka huku akianza kubadilika usoni taratibu, uwoga mwingi ulimtawala akakosa kujiamini nadhani hata moyoni alijuta kurudi tena ndani.
Niliona kuwa huyu keshavurugwa saikolojia hivyo njia kumuweka sawa nilijua nini nifanye, nilichokifanya nilimsukumia kitandani akalala chali nami nikaja juu.
Nilifanya kila namna, niliongea kila aina ya sauti nilifanya kila aina ya utundu hatimae kile kiwewe kilichokuwa kimemtawala kikamtoka akatawaliwa na huba, akili yake ikajaa kila aina ya uzinifu hapo ndipo nikamwachia ili anitawale.
Kweli hakushindwa alinitawala na akanimudu vyema sana alinipeleka palefu saana nilitalii kila aina ya vilima na mabonde...
Safari iliyodumu dakika nyingi tuu! Hatimae sote kwa pamoja tukajipongeza kumalizia safari na kufika salama juu ya kilele cha mlima HUBA!
Jr alishuka akalala chali kwanza huku akiwa kachoka mno! Mimi sasa ndiyo usiseme!
Dah! Halafu kuna muda nilianza kujionea aibu kwa kitendo cha kugawa penzi kirahisi kabisa pasipo kutamkiwa hata neno moja la kutongozwa!
Nilihisi huenda kuna kudharaulika, hata hivyo sikutaka hayo mawazo yakitawale kichwa changu niliyatupilia mbali.

“Eti Jr!”
“Mmh!”
Aliitika kwa kuguna.
“Vipi unajisikiaje?”
“Najisikia furaha sana,lakini pia najisikia kuchoka kiasi.”
“Hongera pia kwa kazi nzuri, hata mimi licha ya kuchoka kiasi lakini pia najisikia furaha kubwa sana.”
“Asante… Ila nikuulize kitu?”
“Uliza.”
“Nini hatima ya hiki kilichotokea?”
“Mmh! Nafikiri ni hatma endelevu inategemea na jinsi tutakavyoendelea kuishi… Hata huu siyo wakati sahihi kulizungumzia hili tutalitafutia wakati sahihi,vipi hivi kwanza imekuwaje hadi nipo hapa?”
Nilimuuliza swali hilo kimtego tu.
“Muda wa mwisho ulizidiwa na pombe sasa wakati nikiwa kwenye harakati za kumtafuta mhudumu wa vyumba ili akupeleke kwenye chumba, ghafla kuna vurugu zilitokea huko nje polisi na panya road walifumaniana wakaanza kujibizana kwa risasi sasa kwa usalama wa wateja ilibidi Dj wa muziki atangaze kupitia spika za baa kuwa watu watoke eneo la ukumbini kwa sababu majambazi wana tabia za kupiga risasi kumbini kupitia madirishani ikabidi nikubebe mkukumkuku hadi huku ndani kukuokoa.”
Nilikuwa nikimsikiliza kwa makini sana...
Lakini kabla sijazidiwa na pombe kuna tukio Jr alilifanya bahati mbaya nilikuja kushitukia mwishoni nikashindwa kujitetea sababu ya kuzidiwa na pombe!
Zile value mbili za mwisho nilizoshiriki kunywa glasi ya mwisho nilitiliwa dawa ya usingizi sasa mwanzo sikustuka ila nilikuja kushtuka mwisho baada ya kuona kichwa kinakuwa kizito kila sekunde iliyogonga na kupotea.
Hata nilipotambua hilo nilishindwa kufanya chochote kwa sababu tayari nilishakunywa nimezidiwa hata kuongea nashindwa.
Duh! Nilipokumbuka kitendo hicho niliishia kumtizam tu, hata nikashindwa kumuuliza nikampotezea nikapanga kumuuliza siku nyingine akiwa kajisahau.
“Ninashukuru sana kwa kunijali.”
Nilimkumbatia nikam'busu akaridhika.

Baada ya hapo tukaingia bafuni tukaoga baada ya hapo mi nilienda chumbani kwangu nikaenda kubadilika, nikavaa nguo zingine safi na kiatu bomba, kuangalia kwenye mkoba niliona nimepungukiwa na pesa za matumizi hivyo nilipanga kupita kwa wakala nitoe kiasi kidogo kitakachonilinda siku hiyo.
Halafu pia nilipanga kuwatafuta wale madalali kwenye simu ili nifike kwenye ofisi zao niweze kuinunua hiyo gari niliyoisikia ikiuzwa na nikaitamani niliomba sana asitokee mtu mwenye pesa akainunua.
Nilitamani sana niikute hiyo gari, kwanza nilianza kupiga hesabu za mbali sana niliona kuwa na gari ningefanya kazi yangu kwa urahisi mno.
Ikumbukwe kuwa ukiachana na kumwondoa ulimwenguni Damson Mbarangu pia kuna kazi ya pesa nyingi sana ilikuwa mbele yangu hivyo licha ya ugumu wa kazi bado nilitakiwa kupambana nifanikishe mapema kabla wanausalama wa Dar es salaam hawajashituka kuwa kuna mamluki kaingia ndani ya mji.
Muda mfupi baadae nilitoka nikiwa tayari nikiwa nimejipara vya kutosha mkoba wangu ubavuni kama kawaida ndani ukiwemo mguu wa bata kwenye kifuko cha peke yake.
Jr nilimkuta ukumbini tayari yuko na safari moja mkononi, na mimi nilifika nikaagiza moja nikainywa ili kupunguza uchovu wa pombe za jana usiku mwilini.
Baadae tuliondoka ,nilichokifanya nilimpatia shilingi elfu ishirini kama nauli huku nikimsisitiza ajitahidi sana kuwa hewani kwani ninaweza kumpigia simu muda wowote ofisi ikinipa gari.
Akanihakikishia kuwa hatoniangusha.
Basi tuliachana nilipanda bajaji iliyonifikisha mpaka barabara kuu hapo nilisimama sehemu ili nitoe simu nipige ofisi ya madalali kama jinsi nilivyokuwa nimepewa maelekezo.
Kitendo cha kutoa simu na kutoa kufuli ya skrini nilishituka kuona picha ya pazia yaani (wallpaper) ikiwa imebadilika kutoka niliyokuwa nimeweka hadi ya majengo fulani ya kutisha!
Ee! Nilishtuka kuinua macho nikashituka zaidi kuona niliposimama pia mji ni ule niuonao kwenye picha ya pazia kwenye simu.
Ulikuwa ni mji mkubwa wenye majengo makubwa yaliyojengwa kimaajabu mno! Kama kawaida gari zilikuwa zikipishana taratibu kwa miendo ya adabu!
Mji haukuwa na mtu yeyote aliekuwa akitembea kwa miguu, isipokuwa magari tu! Nayo yalikuwa mengi sana!
Anga la mji ule lilitisha kwa kweli hakukuwa na jua liwakalo bali kulikuwepo na gimba mfano wa mwezi lililokuwa likitoa mwanga laini sana.
Nikiwa bado ndani ya mshangao ghafla gari ilifika ikasimama mbele yangu, milango ikajifungua nikashituka sana kumuona Sam akiwa ndani ya gari, wakati milango inafunguka macho yetu yaligongana moyo ukapiga paah! Nikameza mate mepesi ya uwoga halafu yeye ndiyo kwaanza akawa ananitizama kwa macho ya tabasamu kubwa sana!
“Karibu kwenye gari mke wangu.”
Aliongea!
Sauti yake tu japo ilikuwa ya upole lakini iliyatetemesha maini yangu, hata hivyo sikuwa na namna niliingia garini huku nikiwa na wasiwasi mwingi sana tayari akili yangu ilishahisi kuwa tayari kiumbe yule ameshajua kuwa nimemsaliti.

Sehemu 28 Sehemu 30
0
0